Gerard Soete |
Wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa huenda wakajiuliza ni vema kumpa sifa japo kidogo kwa mwanajeshi, mwandishi wa vitabu na Mwalimu wa Ubelgiji Gerard Soete kwa kulihifadhi jino la dhahabu la mwanasiasa aliyeipambania Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutoka katika makucha ya Ubelgiji Patrice Lumumba au aachwe hivyo hivyo? Hapo wanatofautiana katika utoaji wa maoni hayo.
Soete kwa sasa hayupo duniani baada ya umauti kumkuta miaka 38
baada ya kutekeleza mauaji ya Lumumba mnamo mwaka 1961.
Baada ya kutekeleza mauaji ya Lumumba Soete alisalia nchini humo
kwa miaka 10 enzi za utawala wa Mobutu Sese Seko kisha akarudi Bruges alifanya
kazi ya ualimu wa lugha katika Chuo cha Mt. Leo
Alizaliwa Januari 29, 1920 huko Pittem nchini Ubelgiji na
kufariki dunia Juni 9, 1999 katika viunga vya Sint Kruis, Bruges katika jimbo
la West Flanders nchini humo kwa kile kinachoelezwa ugonjwa wa moyo.
Mjadala huo mpana unakuja wakati sherehe rasmi za maziko kwa
jino la Lumumba zimefanyika Juni 30, 2022 kwenye mji mkuu wa taifa hilo
Kinshasa.
Mabaki hayo ya jino ni ya waziri mkuu wa kwanza wa nchi hiyo ya
Kiafrika, ambaye aliuawa mwaka 1961 na waasi waliotaka kujitenga kwa
kushirikiana na mamluki wa Ubelgiji.
Mwili wake uliyeyushwa kwa asidi lakini afisa huyo wa polisi wa
Ubelgiji alilihifadhi jino hilo kama kombe la dunia.
Alipigwa risasi na kuuawa mwaka 1961 na mamluki waliokuwa wakiunga mkono
kwa siri utawala wa ukoloni wa Kibelgiji, mwili wake ulizikwa katika kaburi
fupi.
Kisha mwili wa Lumumba uliondolewa
tena katika eneo hilo na kusafirishwa
kilomita 200 (maili 125 ) kisha akazikwa tena, haikutosha mwili wake
ulifukuliwa na kukatwakatwa vipande na
kutumbukizwa kwenye aside ambako uliteketea wote.
Kamishna wa polisi wa Ubelgiji, Gerard
Soete, ambaye alisimamia na kushiriki katika kuangamiza mabaki alichukua jino,
alikiri baadaye.
Pia alizungumzia kuhusu jino la pili
na vidole viwili vya maiti, lakini hivi havikupatikana.
Kilichopo kwa sasa, mipango inafanyika
kwa ajili ya kulirejesha jino lake kwa familia yake katika sherehe
itakayofanyika katika mji mkuu wa Ubelgiji Brussels.
Soete ambaye alitunza vipande vya mwili ilielezea pia kuhusu tabia ya maafisa
wa kikoloni wa Ulaya ya kurejesha masalia ya mwili nyumbani baada ya miongono
kama kipindi cha kukumbuka kuwa kila mtu lazima atakufa.
Je, wewe una maoni gani kuhusu Gerard Soete
aliyeamua kulitunza jino hilo?
0 Comments:
Post a Comment