Friday, July 22, 2022

Kata, Vijiji vyatakiwa kuendelea kuhamasisha watu kuhesabiwa Agosti 23

Viongozi wa ngazi ya kata na vijiji watakiwa  kuendelea kuhamasisha wananchi kwenye maeneo yao  washiriki kuhesabiwa kwenye Sensa  ya Watu na Makazi itakalofanyika Agost 23 mwa huu.

Hayo yalibainishwa na baadhi ya makarani wa  Sensa  ngazi ya mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kufanya mafunzo ya majaribio  ya kutambua mipaka  ya maeneo wakati wa kuhesabu watu kwenye kata ya Mabogini  iliyopo wilaya ya Moshi vijijini na kata ya Pasua iliyoko halmashauri ya Manispa ya Moshi.

Karani wa sensa Agnes Mchau, alisema mafunzo hayo yalilenga kuandaa dodoso la jamii ili kuona changamoto na huduma zinazopatikana kwenye jamii husika, hivyo akatoa wito kwa viongozi wa kata na vijiji kuendelea kuwahamasisha wananchi washiriki kuhesabiwa.

“Ziara yetu ya mafunzo kwa vitendo yalilenga kuangalia dodoso la jamii ili kuona huduma gani zinazopatikana kwenye jmaii husika, kuna changamoto ambazo tumekutana nazo mfano ramani inakuonesha kwamba eneo hili linatakiwa lianzie hapa na kuishia mahali flani, unapofika katika eneo husika unakuta yule kiongozi anayewaonesha mipaka hiyo anahisi kama mnataka kumnyang’anya baadhi ya mipaka na kuipeleka kwingine,”alisema Agnes.

“Tulikwa kwenye mafunzo kwa vitendo ambapo tulitembelea kata za Kibosho na kata ya Mabogini na Pasua, mafunzo kwa vitendo yalikuwa mazuri, kwasababu yalituimarisha vizuri na tukiri kwamba tulikutana na baadhi ya changamoto kadhaa lakini changamoto hizo zilikuwa sehemu ya kutuimarisha zaidi,”alisema Mwalimu Yateri.

Naye Peter Msaka alisema mafunzo hayo ya sensa kwa vitendo yalikuwa yamelenga makarani kuitambua mipaka ya maeneo husika watakayokwenda kuhesabu watu wakati wa zoezi la sense ya watu itkapofika.

“Kimsingi mafunzo haya yametujengea uwezo wa kutosha kwa kuwa kila karani atakuwa na eneo lake hivyo kwenda kujua eneo lake na mipaka inapoishia ni muhimu, vinginevyo kama atashindwa kuitambua mipaka yake anaweza kusababisha mtu kuhesabiwa mara mbili,”alisema Msaka.

Kwa upande wake Mratibu wa Sensa mkoa wa Kilimanjaro Albert Aloyce Kulwa alisema zaidi ya washiriki 292 wa mafunzo wameanza mafunzo ya majaribio kwa njia ya vitendo ambapo watakwenda katika Kata tatu  za Manispaa ya Moshi pamoja na Kata mbili zilizoko Wilaya ya Moshi Vijijini, ili kuhoji dodoso la jamii, litakaloambatana na  kutambua mipaka  eneo husika, kuzipima nyenzo ambazo wamejifunza kwa vitendo kila mtu aweze kutambua mipaka ya ramani husika.

“Sensa ya Watu na Makazi inasaidia kupata idadi kamili ya watu walio kwenye eneo husika hivyo hata mafungu ya fedha yanayotolewa na serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo yanatoka kulingana na idadi ya watu, hivyo ni lazima wahesabiwe kwa ajili ya maendeleo yao.

Sensa ya mwaka huu itakuwa ya sita  kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 ambapo sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.







0 Comments:

Post a Comment