Mkuu wa Wilaya ya Moshi Abbas Kayanda akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Maimoria Julai 1, 2022 |
Uongozi wa Soko la Maimoria Manispaa ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro umesimamishwa ili kupisha uchunguzi kutokana na kushindwa kutatua kero za wafanyabiashara sokoni hapo.
Hayo yanajiri ikiwa ni siku moja tu baada ya Manispaa hiyo kumpata Meya Mpya Zuberi Abdallah Kidumo aliyechukua nafasi hiyo baada ya Juma Rahibu Juma kuvuliwa.
Kwa muda mrefu wafanyabiashara sokoni hapo wamekuwa wakitoa
malalamiko yao kuhusu hali mbaya ya soko ikiwamo mfanyabiashara mmoja kumiliki
kibanda zaidi ya kimoja kinyume na utaratibu.
Kero nyingine ambayo imekuwa ikitajwa ni wafanyabiashara
walio na uwezo mkubwa kuwagandamiza walio na uwezo mdogo hatua ambayo imekuwa
ikichangia mitafaruku ya mara kwa mara sokoni hapo.
Mwenyekiti William Molel, Makamu Mwenyekiti Jermeia Abraham
Mikumi, Katibu Mahmoud Yahya Furtuni, Katibu msaidizi Mosesi Mayori ndiyo
waliokutwa na kibano hicho ambacho kitawaweka pembeni mpaka uchunguzi
utakapokamilika.
Akizungumza katika sakata hilo, mkuu wa wilaya ya Moshi Abbas
Kayanda amesema;
Hakuishia hapo Kayanda ametaka utaratibu wa mfanyabiashara
mmoja kumiliki kibanda zaidi ya kimoja ufuatwe na sio zaidi ya hapo.
Aidha Kayanda amesisitiza suala la usafi sokoni hapo na
kukomeshwa kwa haraka kwa baadhi ya wafanyabiashara kutokana na tabia ya
kujisaidia ovyo pembezoni mwa eneo hilo ili kuepusha maradhi ya kuambukiza.
Hatimaye, uongozi wa muda wa soko ulitangazwa na Mkurugenzi
wa Manispaa ya Moshi Rashid Gembe ambapo Mwenyekiti Geofrey Mwashiuya na
wenzake walipata fursa hiyo.
Kwa upande wake Mwashiuya baada ya kuteuliwa kushika nafasi
hiyo hadi pale uchunguzi utakapokamilika amesema
Mwenyekiti wa muda wa soko la Maimoria Geofrey Mwashiuya |
Mwenyekiti aliyesimamishwa William Mollel (wa pili kutoka kushoto) |
0 Comments:
Post a Comment