Tuesday, July 19, 2022

Wanafunzi wenye ulemavu Korogwe waomba kujengewa mabweni

Watoto wenye Ulemavu katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mkoani Tanga, wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mabweni, jambo ambalo limechangia kuzorotesha jitihada za kuwapatia elimu.

Taarifa hiyo imetolewa na Afisa Elimu Maalum wa Halmashauri ya Mji Korogwe Janeth Ngowi.

Katika mazungumzo yake na gazeti moja nchini , Ngowi alisema, halmashauri ya Mji Korogwe idadi ya Wanafunzi walemavu waliosajiliwa imefikia 220, huku akibainisha kwamba idadi hiyo ya wanafunzi hao imepatikana kwa kubainishwa baada ya Wazazi na walezi wao kuwafichua mara tu walipoweza kuelimishwa.

Afisa huyo aliendelea kusema kuwa, kwa sasa wanafunzi  hao wamekuwa wakisoma katika shule mbalimbali zilizopo halmashauri ya Mji huo.

Ili watoto hao kuweza kupata elimu kwa usahihi, Ngowi alisema,
wanahitaji nguvu za wadau katika kuwajengea mabweni likiwemo la wavulana na linalowahusu wasichana.

"Tunakabiliwa na changamoto ya namna ya kuwakusanya pamoja na kuwafundisha, tunaomba wadau watakaoguswa watuwezeshe kupata mabweni"alisema Ngowi.

Ngowi alitanabaisha kuwa, hali ya uchumi na ulemavu iliyopo kwa jamii hiyo vimekuwa vikichangangia kuwaathiri kushindwa kuhudhuria masomo
yao kwa ufanisi.

Kwa mujibu wa Ngowi, tayari wamefanikiwa kupata eneo huko Shule ya Msingi Kwamngumi alikoeleza kuwa miundombinu ya maji na nishati ya
umeme vinapatikana kirahisi.

Miongoni mwa wanafunzi hao walemavu, wenye matatizo ya akili ni 138 wavulana 95 wasichana 43,usonji idadi yao ni wavulana 3,vizi wavulana 5 na wasichana ni 4.

Uoni hafifu wapo 30 wavulana 21 wasichana 9,baki usikivu yupo mvulana mmoja wasichana 3,albino wavulana 2 wasichana 4,walemavu viungo wavulana 11 wasichana 8,wasioona mvulana na ulemavu mchanganganyiko wavulana watatu.

0 Comments:

Post a Comment