Wednesday, July 6, 2022

Semina ya Wakufunzi wa sensa ngazi ya mkoa Kilimanjaro yaanza

Semina ya wakufunzi wa sensa  ngazi ya mkoa wa Kilimanjaro imeanza leo Julai 6,2022 kwa washiriki 300 kupata mafunzo hayo ikiwa ni mpango wa kuwajengea uwezo wa kufundisha katika ngazi za wilaya na tarafa.

Mratibu wa sensa mkoa wa Kilimanjaro Albert Aloyce amesema taifa linajiandaa na sensa ya watu na makazi mwaka huu ambapo wakufunzi hao wataenda kuwafundisha makarani na wasimamizi namna ya kutumia vishikwambi katika zoezi hilo.

Hata hivyo watanzania wametakiwa kutoa taarifa sahihi siku ya zoezi la sensa ya watu na makazi ili kuliletea taifa maendeleo kwani utoaji wa taarifa zisizo sahihi zinaharibu mipango ya serikali kuwahudumia watanzania kulingana na idadi yao.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo kuelekea Sensa ya Agosti 23 wamesema yatawajengea uelewa wa kutosha wa zoezi zima bila shaka yoyote na kuongeza kuwa mafunzo hayo yamewashirikisha makundi yote katika jamii wakiwamo wenye ulemavu.

Mafunzo ya siku 21 yanawaleta pamoja wakufunzi hao ambapo Sensa ya Watu na Makazi inatarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

Mratibu wa sensa mkoa wa Kilimanjaro Albert Aloyce 


 

0 Comments:

Post a Comment