Mahakama nchini Ufaransa imemkuta na hatia Rais wa zamani wa taifa hilo Nicolas Sarkozy na kumhukumu miaka mitatu jela.
Sarkozy amekutwa na mashtaka ya rushwa wakati akiwa madarakani. Mahakama imemhukumu Sarkozy na kwamba mwaka mmoja atakuwa jela na mingine miwili atatumikia akiwa nyumbani.
Sarkozy alihudumu katika nafasi ya urais kutoka mwaka 2007 hadi 2012. Majaji walisema ushahidi upo bayana kuhusu mashtaka yaliyomsekwa jela.
Nicolas Sarkozy ni nani?
Nicolas Sarkozy ni mwanasiasa aliyekuwa Rais wa Ufaransa tangu 16 Mei 2007.
Sarkozy ni mtoto wa baba mkimbizi kutoka Hungaria na mama wa asili ya Kiyahudi. Alijiunga na siasa akawa mwenyekiti wa chama cha UMP cha rais Jacques Chirac akateuliwa kuwa mgombea wa chama hiki.
Alizaliwa Januari 28, 1955. Alijipatia sifa ya kuwa mkali dhidi ya wageni na wahamiaji waliovunja sheria akidai kuwarudisha katika nchi walipotoka au hata nchi za mababu.
Sarkozy alipokuwa madarakani aliwastajabisha wengi kwa kuingiza mawaziri kutoka chama cha upinzani katika serikali yake pamoja na mawaziri wenye asili ya Kiafrika na Kiarabu kati yao Rachida Dati (waziri wa sheria), Fadela Amara (waziri msaidizi wa nyumba na maendeleo ya miji) na Rama Yade (waziri msaidizi wa mambo ya nje kwa haki za binadamu).
Mwezi wa Oktoba 2007 Sarkozy alitangaza talaka na mke wake Cécilia Sarkozy atakayeendelea kulea mtoto wao wa pamoja.
0 Comments:
Post a Comment