Tuesday, March 2, 2021

MAKTABA YA JAIZMELA: Miaka 121 ya kifo cha Mangi Meli

Eneo la soko la Tsuduni, Moshi lilikuwa  ni sehemu ya makutano yaliyo unganisha wauzaji na wanunuaji wa chakula, vifaa na bidhaa za kila siku.

Eneo hili lilifunikwa na matawi ya Mgunga mkubwa, na lilizoeleka pia kama eneo la kupokea na kusambaza habari na taarifa mbalimbali.

Hata hivyo kumbukumbu kubwa inasalia ni ile ya Machi 2, 1900 pale Mangi Meli aliponyongwa na kuuawa kikatili kisha kichwa chake kukatwa mbele ya watu wake na Wajerumani. Ikumbukwe kwamba wakati wa mapambano yake dhidi ya majeshi ya kikoloni Mangi Meli alisaidiwa na Jumuiya ya wakuu wenzake (Njama). Wakuu hawa walisimama na Mangi Meli katika maisha yake hadi mauti yalipomkuta.

Sababu kubwa iliyowafanya wahukumiwe kifo ilikuwa ni mipango yao ya kuipindua serikali ya Ujerumani hivyo Mangi Meli na wengine 18 walihukumiwa kwenye tukio ambalo lilishuhudia kichwa chake kikikatwa na kuhifadhiwa kusikojulikana na serikali ya Ujerumani.

Bado jitihada zinaendelea hadi sasa ikiwa ni miaka 121 imepita kutaka fuvu la Mangi Meli lirudishwe katika ardhi yake.

Mangi Meli alizaliwa mnamo mwaka 1866 na kufariki dunia mnamo Machi 2, 1900.

0 Comments:

Post a Comment