Nyota wa zamani wa soka nchini England Glenn Roeder amefariki dunia baada ya kuupigania uhai wake kwa muda mrefu kutokana na maradhi ya uvimbe katika ubongo.
Taarifa za kifo chake zimetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mameneja wa Ligi nchini England (LMA) Howard Wilkinson.
Roeder amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 65. Alicheza kwa mafanikio makubwa kabla hajaanza kuzinoa Watford, West Ham, Newcastle na Norwich City.
Nyota huyo alicheza na nyota wa zamani wa England Paul Gascoigne ‘Gaza’ wakati huo wakihudumu wote katika klabu ya Newcastle United. Alihudumu zaidi ya mechi 500 katika safu ya ulinzi katika klabu mbalimbali zikiwamo Leyton Orient, QPR, Newcastle United na Watford.
Alizaliwa Desemba 13, 1955.
0 Comments:
Post a Comment