Mbio za Kili Marathon 2021 zimefanyika hapo jana mjini Moshi kukishuhudiwa Augustino Paulo Sulle akichukua taji hilo kwa wanaume katika kilometa 42 akitumia saa 02:18:04.
Nafasi ya pili imeshikwa na Michael Kishiba Sanga akitumia saa 02:19:21 na nafasi ya tatu ikikamatwa Charles Sulle aliyetumia saa 02:20:54. Kwa upande wa wanawake Jackline Juma Sakilu alitwaa taji hilo akitumia saa 02:45:44, Catherine Lange Yuku alitumia 02:59:06; Mary Xwaymay alitumia 03:07:28
Hatua ya watanzania hao kuchukua taji hilo katika mbio hizo za 19 tangu kuanzishwa kwake inatokana na Chama cha Soka cha Kenya kuwazuia nyota wake kushiriki mbio hizo kutokana na maradhi ya Covid-19. Wakenya wamekuwa washindani wakubwa katika mbio hizo tangu kuanzishwa kwake.
Hata hivyo matokeo ya mwaka huu kwa watanzania hao yameonekana kuleta ahueni ukilinganisha na mwaka 2020 ambapo muda uliotumika kwa Mtanzania wa kwanza Jackson Makombe ulikuwa saa 02:21:14.
Mkenya Kiplagat Onesmus Kiplimo aliyetwaa taji hilo mwaka 2020 alitumia saa 02:16:56. Kwa upande wa wanawake Lydia Wafula wa Kenya alitumia saa 02:47:05 huku Mtanzania Angel John alitumia saa 03:00:33 na kushika nafasi ya nne akizidiwa na Wakenya.
0 Comments:
Post a Comment