Wednesday, March 3, 2021

Crystal Palace vs Manchester United preview

 

Leo usiku kutakuwa na michezo mingine ya Ligi Kuu nchini humo kukishuhudiwa Burnley wakiikaribisha Leicester City, Aston Villa watakuwa ugenini katika dimba la Bramall Lane kuwakabili wenyeji Sheffield United wanaoburuza mkia katika msimamo wa ligi kuu. 

Macho na masikio yatakuwa katika dimba la Selhurst Park, Kusini mwa London pale Manchester United itakaikabili Crystal Palace iliyo katika nafasi ya 13 na alama zake 33. Palace watakuwa wakitafuta kujiongezea rekodi dhidi ya Manchester United; pia nyota wa Palace Wilfred Zaha anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kuifunga timu yake ya zamani nyumbani na ugenini dhidi ya Mashetani Wekundu. 

Hata hivyo Manchester United haijafungwa mara saba jijini London ikiwa ni rekodi iliyochukua muda mrefu tangu mwaka 2013. United imeshinda mara nne na kutoa sare tatu na timu za jijini London. 

Aidha United imeshinda mechi tisa kati ya 11 za Ligi Kuu ya England ilizocheza katika siku za Jumanne, Jumatano na Alhamisi.

0 Comments:

Post a Comment