Rais wa zamani wa Barcelona Josep Maria Bartomeu na mshauri wake wa zamani Jaume Masferrer wameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na maafisa wa polisi tangu siku ya Jumatatu.
Wawili hao wanahusishwa na kashfa ya Barcagate ambayo lianza kufuatiliwa mnamo Mei 2020. Maafisa wa upelelezi waliwakamata kwa ajili ya mahojiano ambapo Mahakama Kuu ya Haki ya Katalunya ilisema wanatuhumiwa kwa kutokuwa waaminifu wakati wa utawala wao klabuni hapo na madai ya rushwa katika biashara.
Wawili hao walikamatwa siku ya Jumatatu baada ya mkurugenzi wa Barcelona Oscar Grau na Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa klabu hiyo Roman Gomez Punti kushikiliwa kutokana na madai ya kuhusika na ufujaji wa mali za eneo la Mossos d’Esquadra.
Wakati hayo yakijiri Barcelona inashuka dimbani leo kuikabili Sevilla baada ya kuzabuliwa mabao 2-0 katika mzunguko wa kwanza wa nusu fainali ambapo wanaowania nafasi ya Urais ndani ya klabu hiyo Joan Laporta, Victor Font na Toni Freixa watakuwa miongoni mwa watazamaji wa mchezo huo utakaochezwa katika dimba la Camp Nou.
0 Comments:
Post a Comment