Monday, March 8, 2021

Joan Laporta, rais mpya Barcelona apata 54% ya kura zote

Joan Laporta ametangazwa rasmi kuwa Rais mpya wa klanu ya Barcelona kwa mara ya pili baada ushindi alioupata kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita. 


Laporta katika kampeni zake alisema ataendelea kumbakisha nyota wa Argentina Lionel Messi, hatua ambayo ilimpa asilimia 54 ya kura kwenye uchaguzi huo. 


Rais huyo mpya wa Barcelona kwa mara ya pili akiwa na umri wa miaka 58 sasa katika muhula wake wa kwanza ndiye alidaka saini ya kocha Pep Guardiola kwa kipindi cha mwaka 2003 hadi 2010. 


Wakati akiwa klabuni hapo katika muhula wa kwanza ndiye aliyemsajili nyota wa zamani wa Brazil Ronaldinho na nyota wa zamani wa Cameroon Samuel Eto'o. 


Pia akiwa Rais aliisaidia Barcelona kutwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, manne ya La liga na Kombe la Mfalme.


Aidha Messi ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Barcelona waliokuwepo kati ka uchaguzi huo; aliibuka kuwa nyota wa dunia wakati wa utawala wa mzaliwa huyo wa Katalunya ambaye ni mwanasheria kwa taaluma.


Mwaka 2009 aliweka rekodi ya klabu ya kutwaa mataji sita ndani ya msimu mmoja.


Laporta amechukua nafasi hiyo baada ya kujiuzulu kwa Josep Maria Bartomeu Oktoba mwaka uliopita. 


Aidha Laporta alimshinda mpinzani wake Victor Font aliyepata asilimia 30 huku wakimwacha mbali Toni Freixa. 

Wapiga kura 55,611 walishiriki kati ya 109,531 na kwamba uchaguzi huo umefanyika baada ya kuahirishwa mwezi Januari kutokana vizuizi vya maradhi ya Covid-19 vilivyowekwa katika jimbo la Katalunya


0 Comments:

Post a Comment