Monday, March 8, 2021

MAKTABA YA JAIZMELA: Joe Frazier alivyohimitisha safari ya Muhammad Ali 1971

Machi 8, 1971 mwanamasumbwi wa uzito mkubwa wa Marekani Joe Frazier alihitimisha safari ya bondia maarufu kwa wakati huo Muhammad Ali wa kushinda mapigano 31 katika ulingo wa Madison Square jijini New York na kutwaa taji la uzito mkubwa kwa pointi baada ya mizunguko 15 kwenye pambano ambalo lilipewa jina la "The Fight of Century." 

Hapo kabla Muhammad Ali alivuliwa mkanda wa ubingwa wa dunia wa uzito wa juu kwa miaka mitatu baada kukaidi amri ya serikali ya Marekani ya kwenda katika vita vya Vietnam. 


Mabondia hawa hawakuwa wamepoteza pambano lolote na mchezo huo ulitangazwa mubashara duniani kote kupitia runinga. Pia ulihudhuriwa na nyota mbalimbali wa dunia wakati huo Woody Allen, Diana Ross, Dustin Hoffman, Burt Lancaster, Barbra Streisand, Sammy Davis Jr, Hugh Hefner, mwandishi wa vitabu Norman Mailer na msanii wa muziki Frank Sinatra.


Sinatra alikamata vichwa vya habari duniani kwani katika pambano hilo licha ya kuwa nyota alisimama na kamera yake na kupiga pambano namna lilivyokuwa likiendelea.

 
Sinatra alikuwa akipenda sana kupiga picha katika maisha yake na jarida la Life lilimpa nafasi ya kuchukua picha za pambano hilo. Mhariri Mtendaji wa jarida hilo Ralph Graves alizitumia picha nne miongoni mwa alizopiga Sinatra katika jarida la mezi uliofuata ikiwa moja iliyokaa katika ukurasa wa kwanza.


Siku hii ya pambano hilo; Zilikuwa zimebaki dakika 15 ifike saa tano asubuhi kengele ya kuashiria pambano lilianze ilipopigwa ndani ya Araneta Queizone. 


Muhammad Alli kama kawaida yake alianza vurugu zake mapema sana, akimtupia Frazier matusi kabla hata hajaanza kurusha ngumi. Joe alimchekea tu na kumwambia “Huna kitu leo”.


Alli alishinda round ya kwanza na ya pili. Akaanza kwa kasi round ya tatu akiendelea kumtukana Joe na kumuambia maneno ya kejeli kama “nipige kwa nguvu nyani wewe.. tatizo ngumi zako laini kama za mke wangu. nakuambia ntakuua leo”. Ila ni katika round ya tatu Joe alifanikiwa kuingiza ngumi ya kwanza kwa Alli.


Frazier aliendelea kumuwashia moto Alli katika round tatu zilizofuata. Alli akarejea kutawala round ya saba na ya nane. Katika round ya tisa Alli alikimbilia pembeni na kumuambia ‘corner man’ wake “ndugu yangu nakufa, kweli tena nakufa kabla sijaandika urithi”. 


Upande mwingine wa ulingo Joe Frazier alikuwa anaugulia maumivu ya uso uliovimba kiasi cha kumziba jicho lake la kushoto.


‘Corner man’ wa Frazier alitupa taulo ulingoni katika round ya 14, japo bondia wake alishinikiza anataka kuendelea. Baada ya pambano Joe Frazier alisema “kweli yule jamaa ni shujaa, nimempiga ngumi zinazoweza kudondosha ukuta, ngumi zinazoweza kumdondosha farasi asinyanyuke tena”.


Alli yeye alisema, “sijawahi kusogelea kifo kama leo, Frazier alikubali yaishe sekunde kadhaa kabla yangu”.


Mnamo Aprili 29, 1967;  bondia Muhammad Ali alikataa kujiunga na jeshi la Marekani kwa ajili ya kuwania mkanda,  kwani walimtaka acheze pambano hilo akiwa mwanajeshi.


Muhammad Ali anachukuliwa kuwa bondia wa kiwango cha juu wa zama zote akitwaa medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki na tuzo nyingine.


Medali ya dhahabu aliyoitwaa bondia huyo ilikuwa katika michuano ya Olimpiki ya mwaka 1960 nchini Italia akiwa na timu ya taifa ya ngumi ya Marekani.


Akiwa na  kimo cha futi 6 na inchi 3 alimkung’uta bondia wa Poland Zbigniew Pietrzkowski na kutwaa medali jijini Rome. 


Ali alikuwa akijulikana kwa makonde yenye nguvu na  namna ya kusimama ulingoni hadi kumtandika mpinzani wake.


Bondia huyo aligundulika kuwa na kipaji cha kucheza masumbwi akiwa na umri wa miaka 12, baada ya baiskeli yake kuibiwa.


Muhammad Ali akitumia jina la Cassius Marcellus Clay Jr. alikwenda kutoa taarifa kwa Afisa wa Jeshi la Polisi Joe Martin kuwa anataka ampige mwizi wa baiskeli hiyo.


Joe Martin alimwambia kuwa atatakiwa kujifunza kupigana kwanza kabla hajakutana na wabaya wake.


Muhammad Ali alizaliwa Januari 17, 1942.



0 Comments:

Post a Comment