Alipata elimu ya msingi katika shule ya Pandani na baadaye Sekondari ya Fidel Castro, Chake Chake, Kusini Pemba.
Baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa Shahada ya Kwanza katika Sheria (LL.B). Baada ya Chuo Kikuu alirejea Zanzibar na kuajiriwa na SMZ katika Wizara ya Katiba na Sheria kama Wakili. Kisha akaenda kusoma Chuo Kikuu cha London ambako alipata Shahada ya Pili ya Sheria (LL.M).
Baada ya masomo aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Utawala Bora na Sheria chini ya Dk Salmin Amour, baadaye akawa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar chini ya Amani Karume na Mwanasheria Mkuu wa Serikali chini ya Dk Mohamed Shein.
Wakati wa Bunge la Katiba, msimamo wake ulimfanya afukuzwe katika CCM, kisha kupoteza wadhifa wake wa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
Agosti 2014 alijiunga na CUF hadi mwaka 2020 alipohamia ACT-Wazalendo. Hatimaye leo ametangazwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
CHANZO: Mwananchi
0 Comments:
Post a Comment