Wednesday, March 3, 2021

Gabriel Jesus atupia mawili Man City ikiizabua Wolves 4-1

 

Mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus amefunga mabao mawili akiisaidia Manchester City kuendeleza rekodi ya ushindi mara 15 mfululizo katika mashindano yote wakiizabua Wolverhampton Wanderers walipokuwa nyumbani Etihad.

Mpira wa chini katika dakika ya 15 ya mchezo uliomiminwa na nyota wa Algeria Riyad Mahrez uliwapa uongozi Man City baada ya mchezaji wa Wolves Leander Dendoncker kujifunga.

Mlinda mlango wa Wolves Rui Patricio aliokoa michomo mingi katika kipindi cha kwanza iliyoelekezwa kwake ukiwa wa Bernado Silva hivyo kuifanya Man city kwenda mapumziko ikiwa na bao moja. Hata hivyo kipindi cha pili mambo yaligeuka na kuleta mabao manne huku Wolves wakifanikiwa kusawazisha bao moja katika dakika ya 61 Conor Coady akirudisha matumaini ambayo hayakudumu akipokea mpira mrefu uliomiminwa na kiungo wa Ureno Joao Moutinho.

Bao jingine la Man City lilifunga na Mahrez huku msumari wa mwisho katika dakika za nyongeza ukikomelewa na Jesus. Man city ipo kileleni kwa pengo la alama 15 ikiwa mbele kwa  mchezo mkononi dhidi ya mahasimu wao Manchester  United waliopo nafasi ya pili. Wolves wanasalia nafasi ya 12 wakiwa na alama 34. 


 

0 Comments:

Post a Comment