Thursday, March 4, 2021

MAKTABA YA JAIZMELA: Erick Lamela ni nani?

Machi 4, 1992 alizaliwa mchezaji wa soka wa Argentina na klabu ya Tottenham Spurs Erik Lamela. Lamela alizaliwa kwa wazazi Miriam na Jose Manuel Lamela katika kitongoji cha kaskazini mwa jiji la Buenos Aires nchini Argentina. Familia yake ilimpa jina la utani ‘Coco’. 


Alijiunga na klabu ya River Palte akiwa na umri wa miaka saba. Aidha Barcelona iliripoti kuwa iliMPA Lamela na familia yake akiasi cha pauni laki moja kwa mwaka pia makazi ya kuishi na ajira kwa wazazi wake ili wahamie jijini Barcelona ukiwa ni mpango sawa na ule uliofanyika kwa nyota Lionel Messi alipokuwa mdogo kwenda nchini Hispania. 


Mnamo mwaka 2004 kikosi cha watengenezaji wa filamu cha Trans World Sport kilisafiri hadi Argentina kwa ajili ya kufanya mahojiano na Lamela wakati huo akiwa na umri wa miaka 12 ambaye alikuwa katika vichwa vya wengi baada ya kufikisha kufunga mabao 120 kwa klabu ya vijana ya River Plate katika msimu mmoja nyuma. 


Katika mahojiano yake Lamela aliweka bayana kuwa anatamani kufuata nyayo za mkongwe na kioo cha soka cha Argentina na dunia Diego Maradona ikiwamo kushinda kombe la dunia. 


Nyota huyu ambaye hucheza katika nafasi ya kiungo alianza maisha yake ya sokas katika klabu ya River Plate ya nchini mwake na mnamo mwaka 2011 alisaini kuitumikia AS Roma ya Italia kwa mkata wa awali wa euro milioni 12. 


Baada ya misimu miwili ya kuwepo Serie A alijunga na Spurs kwa ada ya pauni milioni 25.8. Alianza kuhudumu na timu ya taifa kuanzia mwaka 2011 na alikuwa miongoni mwa wachezaji walioshiriki kuisaidia timu ya taifa ya Argentina kumaliza nafasi ya pili katika mashindano ya Copa America mnamo mwaka 2015 na 2016. 

Mnamo Novemba 2018 aliitwa tena katika kikosi cha Albicelestes ikiwa ni miaka miwili ya kutokuwamo kikosini humo. Hadi sasa ameifungia timu ya taifa mabao 3 katika mechi 25 alizocheza.


Mnamo Agosti 30, 2013 klabu ya Tottenham ilikamilisha usajili wa Lamela kutoka AS Roma  na kumpa bonsai ya pauni milioni 4.2. Ada aliyonunuliwa Lamela ilimfanya wakati huo kuwa mchezaji ghali katika historia ya klabu hiyo akivunja rekodi mbili za usajili ghali zilizowekwa na klabu hiyo walipowasajili Paulinho na baadaye Roberto Soldado.


Mpaka sasa Lamela amecheza mechi 168 akiwa na Majogoo hao wa London na kufumania nyavu mara 16; ambapo msimu wa 2020-21 Lamela alianza katika robo fainali ya Kombe la Ligi (Carabao) dhidi ya Chelsea. 

Aliisawazisha Spurs ikiwa ni bao lake la kwanza la msimu na baada ya hapo alifunga penati kwenye ushindi wa mikwaju 5-4 baada ya sare ya 1-1. Mnamo Januari 2021,  alipigwa faini baada ya kuvunja sheria iliyowekwa ya kujikinga na maradhi ya Covid-19 baada ya kuhudhuria sherehe za Krismasi na aliwekwa  pembeni katika kikosi cha Spurs kwa mechi kadhaa. 


Lamela ana watoto wawili Tobias (2017) na Thiago (2020) aliowazaa kwa kipenzi wake wa siku nyingi Sofia Herrero.

0 Comments:

Post a Comment