Leo jumatatu kutashuhudiwa timu ya taifa Uganda chini ya umri wa miaka 20 maarufu The Hippos au Viboko ikishuka dimbani katika nusu fainali dhidi ya Tunisia.
Kuelekea mchezo huo hapo baadaye kocha wa Uganda Morley Byekwaso amesema kikosi chake kinaweza kuwa mabingwa wa taji hilo mwaka huu kutokana na hatua zake za kustaajabisha ambazo hakuna aliyetegemea kama ingeweza kufika hatua hiyo.
Uganda itakabiliwa na timu yenye uimara ya Tunisia ambayo iliingia katika hatua hiyo baada ya kuizabua Morocco kwa changamoto ya mikwaju ya penati mwishoni mwa juma lililopita huku Uganda ikizama hatua hiyo baada ya ushindi wake dhidi ya Burkina Faso.
Uganda itajivunia nyota wake katika nafasi ya kiungo mwenye umri wa miaka 18 Bobosi Byaruhanga anayehudumu katika klabu ya Vipers huku Tunisia ikiegemea kwa mshambuliaji wa Sheffield Wednesday Hassan Ayari na kiungo wake Chiheb Labidi.
Kwa upande wake Kocha wa Tunisia Maher Kanzari amesema wanachukulia kila mchezo kama fainali, huku wakisahau furaha na machungu ya michezo iliyopita. Kanzari hakusita kuisifia Uganda kutokana na uimara walionao na kuongeza kuwa utakuwa mchezo mgumu.
0 Comments:
Post a Comment