Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amesisitiza kuwa nyota wake Gareth Bale yuko vizuri kuliko wakati mwingine wowote aliowahi kucheza katika soka na kuongeza kwamba hakuna kocha yeyote duniani atakayemkataa mshambuliaji huyo kutokana na kiwango alichokionyesha dhidi ya Burnley walipoibamiza kwa mabao 4-0.
Nyota huyo wa Kimataifa wa Wales alionyesha uwepo wake katika kikosi cha Spurs sio bure tangu alipotua akitokea Real Madrid kwenye ushindi huo dhidi ya Clarets.
Katika mchezo huo Bale alifunga mabao mawili akitoa pasi ya mwisho moja iliyofungwa na Harry Kane na akipiga pasi 33 zilizokamilika kati ya 42 alizopiga. Aidha Bale aligusa mipira 52 katika mchezo huo ukishuhudiwa Lucas Moura naye akifunga miongoni mwa mabao hayo.
Aidha hapo jana kulishuhudia Arsenal ikiilaza na viatu Leicester City kwa mabao 3-1. Liverpool ikipunguza pengo kuikaribia nne bora baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sheffield United.
Crystal Palace na Fulham zilitoka sare tasa huku kocha wa Manchester United Ole Gunner Solskjaer akiwavimbia waamuzi kwa hasira baada ya kulazimishwa sare tasa dhidi ya Chelsea.
Leo Everton na Southampton pale Goodison Park. Miamba hii imekutana mara 43 katika mechi za Ligi Kuu ikitoka sare mara 12 huku Everton ikishinda mara 18 dhidi ya 13.
0 Comments:
Post a Comment