Machi 1, 1949 ni siku ambayo mwanamasumbwi mahiri nchini Marekani aliyefahamika kwa jina la Joel Louis alistaafu medani ya ndondi.
Louis alikuwa bondia wa uzito mkubwa alistaafu akiwa na umri wa miaka 35. Jina lake halisi ni Joseph Louis Barrow ambaye alipata umaarufu na kupachikwa jina la Brown Bomber.
Huyu anashikilia umaarufu wa uzito mkubwa katika nafasi ya pili baada ya Muhammad Ali katika historia ya mchezo huo nchini Marekani.
Alizaliwa Mei 13, 1914 huko Alabama na kufariki dunia mnamo Aprili 12, 1981 huko Paradise jimboni Nevada. Alikuwa katika medani ya ushindani kutoka mwaka 1934 hadi 1951. Alitawala taji hilo kutoka mwaka 1937 hadi 1949 ambapo akishiriki mapigano 69 akishinda 66 na kupoteza matatu. Katika hayo aliyoshinda mapigano 52 alishinda kwa KO.
Pambano lake la kwanza alishinda kwa KO dhidi ya bondia wa Norway Jack Kracken mnamo Julai 7, 1934.
Mapambano matatu aliyoyapoteza alipanda uingoni dhidi ya Ezzard Charles maarufu Cincinnati Cobra mnamo Septemba 27, 1950, Max Schmeling mnamo Juni 19,1936 na Rocky Marciano mnamo Oktoba 26, 1951 ambalo lilikuwa pambano lake la mwisho.
Pia nyota huyo anashikilia rekodi ya kushinda mataji 25 mfululizo ambapo mnamo mwaka 2005 alitunukiwa heshima ya kuwa mwanamasumbwi wa zama zote na Shirika la Kimataifa la Utafiti katika Ndondi (IBRO) na pia aliingia katika orodha ya wapiganaji 100 bora wa mchezo huo wa zama zote na Jarida la The Ring.
Louis anaendelea kushikilia rekodi ya kuwa bondia pekee aliyeshikilia ubingwa wa uzito wa juu kwa muda mrefu.
Aidha maisha yake nje ya ulingo yalikuwa mazuri huku akichukuliwa kama mtu wa kwanza Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika kuwa shujaa ulingoni. Aidha Louis aliangaliwa kwa jicho la tofauti kama mtu aliyekuwa kinyume na utawala wa Kinazi wa Adolf Hitler na pia wakati wa vita vya Pili vya dunia alirudi ulingoni kupambana na bondia wa Kijerumani Max Schmelling mnamo mwaka 1938.
Pia alivunja ukuta wa rangi katika michezo pale alipozama katika mchezo wa gofu bila kizuizi cha mdhamini wa mashindano ya PGA mnamo mwaka 1952. Hadi anafariki dunia alikuwa na watoto wawili Jacquilline na Louis Jr. aliowazaa kwa mkewe Marva Trotter waliyetalikiana mnamo mwaka 1949.
0 Comments:
Post a Comment