Everton watakuwa na kibarua dhidi ya Wes Brom ambako wataikosa huduma ya Yerry Mina, Fabian Delph na Jean-Philippe Gbamin ambao wanaendelea kuuguza majeraha yao.
Aidha Kocha Carlo Ancelotti ameweka bayana kuwa nyota wake James Rodriguez, Seamus Coleman, Tom Davies na Robin Olsen watachunguzwa kama wataweza kuwavaa The Hawthorns katika mchezo wa leo usiku.
Kwa upande wao West Brom, kiungo wao Robert Snodgrass atakuwamo katika mchezo wa leo baada ya kupona majeruhi ya goti na kigimbi yaliyokuwa yakimsumbua.
Hata hivyo mshambuliaji Dominic Calvert-Lewin atahitaji kufunga bao moja tu leo katika mchezo wa ugenini ili kufikia rekodi ya Romelu Lukaku aliyoiweka ya kufunga mabao tisa ugenini katika Ligi Kuu wakati akiwa hapo.
0 Comments:
Post a Comment