Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameondoka
nchini kwenda Afrika ya Kusini ambapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa
kwa Rais Mteule wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa.
Katika safari hiyo Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Philip Mangula na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi.
Wakizungumza kabla ya kuondoka, Rais Mstaafu Kikwete na
Makamu Mwenyekiti wa CCM Mangula wamesema Tanzania na Afrika ya Kusini zina
uhusiano mkubwa na wa kihistoria na kwamba Serikali na chama zina kila sababu
ya kudumisha uhusiano na ushirikiano huo.
Viongozi hao wameondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa
kwa Rais Mteule wa Afrika ya Kusini, Rais Magufuli atafanya Ziara Rasmi ya
Kitaifa nchini Namibia ambako pia atazindua mtaa uliopewa jina la Baba wa Taifa
Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kutambua
0 Comments:
Post a Comment