Wakati klabu ya Manchester City wakiendelea kuufurahia ubingwa wa Ligi Kuu ya England wamiliki wa klabu ya Brighton Hoves & Albion wamemtimua kocha wao Chris Hughton licha ya kunusurika kushuka daraja.
Brighton ilizabuliwa mabao 4-1 na Manchester City katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Uingereza wikiendi iliyopita. Hughton ametimuliwa akiwa aliiongoza kwa mara ya kwanza kuwa kuzama Ligi Kuu baada ya miaka 34 mwaka 2017. Aidha Brighton imeshinda mechi tatu pekee katika michezo 23. Graham Potter anaangaziwa kuchukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo.
|
Chris Hughton ndiye kocha wa mwisho kuisimamisha Man City katika mechi ya mwisho ya msimu 2012/2013 |
|
Man City wakishangilia ubingwa baada ya kuinyuka Brighton Mei 12, 2019 |
0 Comments:
Post a Comment