Tuesday, May 7, 2019

Maadhimisho ya Wakala wa Vipimo Mei 20



WAKALA wa Vipimo (WMA) inatarajia kuweka Sticker katika vipimo mbalimbali ili kuweza kumlinda mlaji kwa huduma inayoendana na thamani fedha yake.

Akizungumza na waandishi wa habari  mjini Moshi , Meneja wa Vipimo mkoa Kilimanjaro  Ephraim Assenga amesema uwekaji Sticker utaanza rasmi Mei 14 mwaka huu kwa kubandika sticker hiyo kwa kila kipimo ambacho kinatambulika na Wakala Vipimo.

Amesema sticker hizo zitawekwa katika pampu zinazotumika katika vituo vya vya mafuta ambavyo vitakuwa vimehakikiwa ili mteja ajue uhalali wa kipimo hicho na mafuta.

“Kila mwaka ifikapo Mei 20 wakala wa vipimo hufanya maadhimisho ya siku ya vipimo duniani ambayo huadhimishwa kwa kufanya shughuli mbalimbali zinazoendana na majukumu ya vipimo ikiwamo  ukaguzo wa mizani midogo katika masoko, ukaguzi kwenye vituo vya mafuta,”  alisema Assenga.

Assenga alisema mlaji akiona sticker katika kituo cha mafuta afahamu kituo hicho kimehakikiwa na wakala wa vipimo. 

Aliongeza kuwa katika uwekaji wa sticker huo utafanywa pia makao makuu jijini Dar es Salaam katika bohari za Mafuta kwa kuweka sticker maalumu katika kipimo cha mafuta 'flow Meters' zitakazotumika kujaza mafuta katika magari ya kubebea mafuta itafanya wabebaji wa mafuta kwa magari wataweza kutambua kipimo hicho kilivyohakikiwa.

Hata hivyo meneja huyo wa mkoa alisema jitihada hizo hufanya uhakiki wa mizani yote kuhakikisha inapima kwa usahihi ikiwa ni pamoja na kuweka sticker maalumu.

Aliongeza kuwa watahakiki mizani ya wafanyabiashara na mizani ambayo itakuwa haina sticker wakulima wasitumie na wanatakiwa kutoa taarifa.

 Pia maeneo mengine watakayofanya ukaguzi katika wiki ya vipimo ni katika maeneo ya viwandani. Kilele cha maadhimisho hayo ni Mei 20 mwaka huu.

STORY BY: Jabir Johnson
EDITED BY: Jabir Johnson/Kija Elias

0 Comments:

Post a Comment