Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira akigawa maziwa kwa watoto wa Shule ya Muungano iliyopo Manispaa ya Moshi katika Uzinduzi wa Jukwaa la Maziwa mkoa wa Kilimanjaro Mei 10, 2019. |
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Muungano wa vyama vya Ushirika wa Maziwa Mkoa wa Kilimanjaro (KDCJE) Nancy Manasseh Kidin, wakati alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta ya maziwa, mjini Moshi mkaoni Kilimanjaro.
“Maziwa mengi yaliyopo katika mkoa wa Kilimanjaro yapo katika mfumo usio rasmi licha ya sheria ya maziwa ya mwaka 2003 na 2006 lakini maziwa yanauzwa bila utaratibu,”alisema .
Alifafanua kuwa "Maziwa ni chakula ni kinywaji, ni lazima yakaguliwe kama ambavyo wataalam wa afya wanavyokagua nyama, lakini kutokana na kutokuwa na usimamizi mathubuti bado maziwa yamekuwa yakiendelea kuuzwa kiholela jambo ambalo hatari sana kwa walaji," alisema Kidini.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema kuwa kinachokatisha watu wengi tamaa ya kutokunywa maziwa ni kwamba maziwa mengi yanayouzwa katika mfumo usio rasmi si maziwa halisi kwa kuwa wafugaji tayari huwa wamekwisha yachakachua kwa kuongeza maji.
“Maziwa yakishafika kwa wafanyabiashara hupenda kuchukua maziwa hayo kiasi kidogo na kuchanganya na unga wa ngano kisha wanatia na mafuta kidogo ili kupata utando wa mafuta juu yake,”alisema Kidin.
Akizungumzia kuhusiana na Muungano huo, alisema lengo la jukwaa hilo litakuwa ni kuwaleta wadu wote wa sekta ya maziwa mkoa wa Kilimanjaro na nje ya mkoa ili kuweza kujadili mwenendo mzima wa sekta ya mazima ikiwemo changamoto na fursa za kiuwezeshaji katika sekya hiyo ya maziwa.
“Kwa sasa ni sera pia ya serikali ya awamu ya tano, ambayo inawataka wafugaji kujiunga katika vikundi ili iweze kuwahudumia wafugaji wengi kwa pamoja, kwani serikali haiwezi kumhudumia mfugaji mmoja mmoja, na kwamba kupitia vikundi, hivyo tunatengeneza ushirika ili faida inayokuja iweze kumnufaisha kila mmoja,”alisema Kidin.
Akizungumzia mafanikio ya tangui kuanzishwa kwa Muungano huo alisema kuwa, kwa kushirikiana na wadau wa Maenndeleio wameweza kuwajengea uwezo vyma vya ushirika vya maziwa viapatavyo 22.
Mafanikio mengine ambayo (JE) imeweza kutoa ni mafunzo kwa vyama wanachama ya utunzaji wa kumbu kumbu hususan kumbu kumbu ya fedha, ukusanyaji na uuzaji wa maziwa , mfumo wa usammbaji wa vyakula na pembe jeo bora za ng’ombe wa maziwa , kuunganisha vyama baadhi na masoko ya usindikaji wa maziwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira alisema hali ya unywaji wa maziwa katika mkoa huo sio wa kuridhishsha kwani takwimu zinaonyesha kuwa mtu mmoja hunywa maziwa chini ya lita 40 kwa mwaka.
"Hali ya unywaji wa maziwa kwa mtu mmoja bado ni kidogo sana ikilinganishwa na kiwango kinachotakiwa cha lita 200 kwa mwaka kwa mujibu wa shilika la Chakula (WHO)
Takwimu zinaonyesha kwamba Kenya inangoza kwa kunywa maziwa , wakifuatiwa na Uganda na Rwanda licha ya kwamba Tanzania imejaliwa kuwa na mifugoo wengi ambao wanatosheleza kwa mahitaji ya maziwa
Tamasha la Unywaji wa maziwa yaliyosindika mkoani Kilimanjaro liliandaliwa na Maradi wa maziwa kutoka shirika la Maendeleo la Uholanzi SNV, na kuwashirikisha wadau wa sekta ya maziwa kutoka wiya ya Siha na Hai.
STORY BY: Kija Elias & Jabir Johnson
EDITED BY: Jaizmelanews
0 Comments:
Post a Comment