Katika maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari ulimwenguni hapo jana,
kumeripotiwa mtangazaji wa redio nchini Mexico kuuawa.
Kuuawa mwa mwanahabari
huyu kunafanya idadi ya waliouawa nchini humo kufikia wanne. Maafisa wa Polisi
nchini humo wamesema aliyeuawa anajulikana kwa jina la Telesforo Santiago Enriquez
ambaye alivamiwa na mtu aliyekuwa na bunduki katika mji wa Juchitan uliopo
katika jimbo la Oaxaca ambako ndiko redio aliyokuwa akifanyia kazi ya El
Cafetal ilipo.
Mashuhuda wanasema siku za hivi karibuni alipokea vitisho katika simu yake ya mkononi. Enriquez alikuwa akifahamika kwa kutoa taarifa zinazohusu masuala ya rushwa nchini humo.
Taarifa ya Kamati ya Haki za Binadamu ya taifa hilo imesema katika kipindi chake Enriquez alikuwa akifanya uchambuzi na ukosoaji kwa serikali na hivi karibuni alikuwa akifanya uchambuzi kuhusu namna mamlaka za manispaa zinavyochukua rushwa kutoka vyanzo.
Mexico ni miongoni mwa nchi hatari duniani katika tasnia ya habari, ambapo mpaka sasa wanahabari 100 wameuawa tangu kuanza kwa karne ya 21 huku taifa hilo likizongwa na vurugu za mara kwa mara zinazohusiana na biashara haramu ya dawa za kulevya na rushwa katika siasa.
Binamu wa mwandishi huyo Aida Valencia amesema ndugu yake alipigwa risasi ya m domo na moyoni kisha kupoteza maisha, aidha Aida ameongeza kuwa anaamini Enriquez aliuawa kutokana na kazi zake za uandishi wa habari.
Kwa upande wao Kundi la Waandishi wasio na Mipaka limesema Mexico inakuwa nchi ya tatu kwa hatari katika kazi za uandishi wa habari baada ya Afghanistan na Syria.
Santiago Enriquez alikuwa pia mwalimu akijulikana kwa kazi yake katika kutunza lugha za asili na utamaduni wake. Mwakilishi wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa nchini Mexico Jan Jarab amethibitisha kuwa Santiago Enriquez aliuawa wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari.

0 Comments:
Post a Comment