Leo ni siku ya taulo. Siku hii huadhimishwa kwa heshima ya Douglas Noel Adams ambaye alikuwa mwandishi wa essay, mtunzi wa vitabu, mwanamazingira, mbunifu na msanii wa maigizo. Huadhimisha kila tarehe 25 Mei kila mwaka
Douglas anapewa heshima hiyo kutokana na kazi yake ya “The The Hitchhiker's Guide to the Galaxy (HG2G)” ambayo ilipata kurushwa katika Radio BBC 4 mwaka 1978. Douglas alizaliwa Machi 11, 1952 na kufariki dunia Mei 11, 2001.
Katika filamu hiyo ya vichekesho kuna matumizi ya taulo hivyo kutokana na wengi kuvutiwa na vichekesho katika filamu hiyo waliamua kuadhimisha ubunifu wa Douglas katika utunzi wake. Hata hivyo Douglas alitoa kazi yake hiyo katika kategori mbalimbali ya maigizo ya sauti (redio), maigizo katika picha (video) na vitabu.
Pia alifanikiwa kutengeneza video games kupitia kazi yake hii ambayo aliuza mamilioni ya nakala.
Nchini Tanzania
inaadhimishwaje?
Hii ni miongoni mwa siku ngeni kabisa masikioni mwa wengi
kutokana na kutofanywa kabisa, wengi huenda hawamfahamu Douglas Adams na kazi
zake.
Lakini kwa mazingira ya Afrika hususani Tanzania taulo limekuwa likifahamika kwa kazi moja tu ya kujifutia unyevunyevu pindi mtu anapotoka kuoga. Kadri siku zinavyokwenda na mabadiliko ya teknolojia na utandawazi matumizi ya taulo yamezidi kupanuka kutoka kuoga hadi kuingia katika masuala mbalimbali kama vile katika mahoteli, baa na migahawa kwa ajili kukausha na kufutia vifaa mbalimbali.
Hivyo basi katika kuadhimishwa nchini Tanzania wengi ambao wamebahatika kutoa maoni yao katika Kilibreakfast ya Redio Kili FM iliyopo Moshi, Kilimanjaro (Mei 25, 2019) walisikika wakisisitiza usafi wa taulo hilo, baada ya matumizi husika ikiwa ni sehemu ya kusheherekea ‘Siku ya Taulo.’
Mwanadada aliyejitambulisha kwa jina la Jackline Mushi alikaririwa akitoa maoni yake kuwa vijana wa kiume ambao hawajaoa (mabachela) wajitahidi kufanya usafi wa mataulo wanayotumia kuoga, ili kupunguza hatari ya magonjwa. Innocent Mkama Bwire ambaye ni dereva wa pikipiki zenye matairi matatu (bajaji) alisema taulo lake hupita hata mwezi mzima bila kulifua mpaka alione limechafuka.

STORY BY: Jabir Johnson
0 Comments:
Post a Comment