Tuesday, May 7, 2019

MAKTABA YA JAIZMELA: Uchaguzi Mkuu nchini Afrika Kusini Mei 7, 2014



Afrika Kusini ina mchanganyiko mkubwa wa watu. Waafrika asili ni asilimia 80.2, Machotara ni 8.8%, Wazungu ni 8.4%, Waasia ni 2.5%. Wengi (79.8%) ni Wakristo wa madhehebu mengi sana, hasa ya Uprotestanti; Wakatoliki ni 7.1%. Dini nyingine ni: Uislamu (1.5%), Uhindu (1.2%), Dini za jadi (0.3%) na Uyahudi (0.2%). Asilimia 15.1 ya watu hawana dini yoyote.  

Afrika Kusini inaongoza duniani kwa wingi wa watu wenye VVU/UKIMWI: mwaka 2015 walikuwa milioni 7. Mayatima kutokana na ugonjwa huo ni 1,200,000. Kiuchumi Afrika Kusini ni nchi yenye pande mbili kabisa. 

Sehemu ya uchumi ina hali ya kimaendeleo kabisa ikiwa na viwanda na huduma zinazolingana na hali ya juu kabisa duniani; hali ya maisha ya wananchi waliomo katika sekta hii inalingana na nchi kama Australia au Ulaya magharibi. Kwa upande mwingine hali ya maisha ya sehemu kubwa ya wananchi ni umaskini kama katika sehemu nyingine za Afrika au Uhindi wa mashambani. 

Lakini kwa ujumla hali ya maisha iko juu kuliko nchi nyingi za Afrika. Sekta muhimu za uchumi ni migodi ya kuchimba dhahabu au almasi, viwanda na huduma kama benki au bima. Kama nilivyokujuza awali ni kwamba uchaguzi huo ni uchaguzi wa tano kufanyika baada ya mwaka 1994 ambapo ilikuwa mwisho wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi katika taifa hilo. Pia uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza tangu kufariki kwa kiongozi maarufu wa taifa hilo Nelson Mandela. 

Aidha ilikuwa ni mara ya kwanza kuruhusu kura katika uchaguzi mkuu wa Afrika Kusini.  Katika uchaguzi huo chama cha ANC kilipata ushindi wa asilimia 62.1, kikiwa kimeshuka ukilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2009 kilipopata asilimia 65.9. ANC ilikuwa ikiongozwa na Jacob Zuma. 

Nafasi ya pili ilishikwa na chama cha Democratic Alliance kikiwa na mgombea wake mwanamke Hellen Zille na kuzoa asilimia 22.2 ya kura kikipanda kutoka asilimia 16.7 kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2009; na nafasi ya tatu ilishikwa na chaa cha EFF kilichopo chini ya kijana Julius Marema kilichojipatia asilimia 6.4; 

ANC katika uchaguzi huo kilifanikiwa kutwaa majimbo manane kati ya tisa. EFF cha Julius Marema kilijizolea asilimia 10 ya kura katika jimbo la Gauteng, Limpopo na North West hivyo kukishinda chama cha Hellen Zille cha DA. Katika jimbo la KwaZulu-Natal chama cha DA kilifanikiwa kukipiku chama cha Inkhatha Fredom na kushika nafasi ya pili. Jimbo la Western Cape ndilo jimbo pekee ambalo ANC haikufanikiwa kupata uungwaji mkono huko hivyo kupoteza jimbo hilo. 

Chama cha DA kilijipatia asilimia 59.4 ya kura kutoka asilimia 51.5. Novemba 26, 2013 ilipitishwa sheria ya uchguzi ambayo iliwaruhusu raia wa Afrika Kusini waliokuwapo nje ya taifa hilo kujiandikisha na kupiga kura. Pia sharia hiyo mpya ilikataza kupigwa picha karatasi za kura katika uchaguzi huo ili kutovuruga zoezi hilo. 

Siku ya uchaguzi huo vituo 22,264 nchini humo vilifunguliwa kwa ajili ya zoezi hilo. Pia iliripotiwa kuwa vituo vipatavyo 2,449 ambayo ni sawa na asili 11 vilifunguliwa baada ya saa 1:00 asubuhi. 

Vituo vya uchaguzi vilifungwa saa 3 za usiku kwa saa za Afrika Kusini siku hiyo. Kwa ufupi huo ni uchaguzi mkuu mwaka 2014 tarehe kama ya leo nchini Afrika Kusini.

0 Comments:

Post a Comment