Friday, May 31, 2019

ANNA DAVID: Maluweluwe yanavyotishia masomo yake

Anna David
Mwanasaikolojia Gary Collins, raisi wa zamani wa Washauri wa Chama Wakristu cha Marekani, aliulizwa uwezekano kwamba maluweluwe yalikuwa kwa wafuasi na ndiyo yaliyobadili kwa kiasi kikubwa tabia yao. 

Collins alieleza, “Maluweluwe ni matukio ya mtu mmoja mmoja pekee” Kwa asili yake ni mtu mmoja peke yake anaweza kuona luweluwe fulani kwa wakati mmoja. Kwa hakika si vitu ambavyo vinaweza kuonwa na kikundi cha watu kwa wakati mmoja.” Hoja hiyo ya maluweluwe kuwa anaweza kuwa nayo mtu mmoja au wawili katika kundi kubwa la watu ikaungwa mkono na mwanasaikolojia Thomas J. Thorbum kwa kusema, “Haiingii akilini kabisa kwamba … watu mia tano, wenye akili timamu za kawaida wawe wameona aina zote za fahamu, za kuona, kusikia, kutenda – na kwamba zote hizi fahamu ziwe zimetokana na kuona maluweluwe – ndoto za mchana!”

Bado hoja ya maluweluwe kwa tafsiri ya wazungu iko hivyo kwa ulimwengu wa kiafrika imekaaje hiyo, mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Mtwara Erick Thomas katika wimbo wake wa ‘Maluweluwe’ anatafsiri maluweluwe kuwa ni changamoto halisi za mwanadamu katika maisha, yaani mwanadamu anaona mambo katika hali ambayo ni tofauti na matarajio hali ambayo inamchanganya kabisa kufikia malengo. 

Hata hivyo wasanii wengine wa kizazi kipya nchini Tanzania akiwamo Goodluck anajiuliza maluweluwe au ni ndumba (uchawi)? Mtumiaji mmoja wa mtandao wa intaneti anajiuliza nini hiki? “kataka kudaka mpira kaona moto, kataka kupiga mpira kaona paka, sasa sijui ndicho kilichotokea?..." 

Bado hajapata jibu. Hapo ndipo kiini cha Makala haya ambayo yatamwangazia mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Sekondari ya Kikatoliki ya Visitation iliyopo Siha mkoani Kilimanjaro.
Visitation Girls Secondary School, Siha; Kilimanjaro
Anna David (16) amekuwa katika changamoto kubwa hali ambayo imekuwa ikitishia masomo yake katika Shule ya Sekondari ya Kikatoliki ya Visitation iliyopo Siha mkoani Kilimanjaro. Anna alihamia shuleni hapo kwa nia ya kufanya vizuri katika masomo yake kutokana na shule hiyo ya wasichana kuwa na msingi mzuri wa ufundishaji wa wanafunzi. 

Anna anasema, “ Nilikubali uamuzi wa wazazi kunileta hapa lakini nimekuwa nikikutana na mambo magumu ndotoni, sijui ni nini hiki.” Aidha msichana huyo anasema hali hiyop inapomjia hujikuta akipiga kelele hivyo inatafsiriwa na walimu wa sekondari hiyo ya bweni kudhani kukiuka masharti ya shule. 

Mwanafunzi huyo anasimulia kisa kimoja kilicholeta tafrani wakati bweni la shule hiyo lililoshika moto mwanzoni mwa mwaka huu. Anna anasema,Moto uliwaka Jumamosi (siku hiyo bweni lilipokuwa likiungua)…nikawa namuona huyo moto kama kivuli, nikawa nawaambia watu wakawa wananiambia tusali na kuwa na Imani.”   

Pia msichana huyo anasema, “Saa nyingine namuona kwenye ndoto…siku nyingine akaja usiku akanikaba.” Hata hivyo Anna anasema kuna mwanafunzi mwingine ambaye naye aliota kama yeye na akawatahadharisha wenzake kuwa kuna tukio litatokea. 

“ Alituambia wiki hii haitaisha moto utawaka, mtoto huyo yuko form one (jina tunalihifadhi) lakini watu wakapuzia, tukapotezea huyo; siku hiyo ilikuwa jumamosi tulikuwa mimi na mtoto mwenzangu akaniambia njoo uone domu (bweni) la katikati linawaka moto,” anaongeza Anna.
Sophia ambaye ni mama mdogo wa Anna David akizungumza na JaizmelaNews.
Kwa upande wa mama mdogo wake ambaye alijitambulisha kwa jina la Sophia, alisema waliitwa shuleni mara mbili kutokana na tabia ya ghafla iliyojitokeza ya kupiga makelele. “Tuliambiwa kuwa Anna anapiga makelele anawafanya wenzie wasisome, anawasumbua kwa ujumla..ikabidi tufike shuleni na kumchukua,” alisema Sophia.
Sophia anasema baada ya kutoka naye shuleni walikwenda naye katika nyumba za ibada kwa ajili ya maombi kwani katika maisha yake tangu amezaliwa hawajawahi kumuona akisumbuliwa na hali hiyo. Aidha mama mdogo huyo anasema kabla hawajamrudisha shuleni wakapigiwa simu kutoka shuleni kuwa binti yao anahusika na uchomaji wa bweni. 

“Tukaamua tumpeleke kwenye maombi, akapata matibabu kabla hajapona tukapigiwa simu kuwa kuna kikao baada ya kufika tukaambiwa kuwa Anna hatakiwa kwani ndiye aliyechoma mabweni,” anaongeza Sophia. 

Hata hivyo familia ya binti huyo wa kidato cha kwanza inadhamiria kumuondoa shuleni hapo kutokana na changamoto hiyo ifikapo mwezi wa saba. 

Mbali na hali hiyo makala haya yalimtafuta Mhubiri wa Injili Zakaria Misitu ambaye alisema, “ Mtu anapotokewa na hali hiyo, cha kwanza ni kumfanyia maombi kwani hakuna linaloshindikana kwa Mungu na pia ushauri nasaha unapaswa kuendelea kufanywa kwa mtu wa jinsi hiyo ili roho chafu zisiweze kumrudia.”
Geti la kuingilia la Visitation Girls Secondary School.

0 Comments:

Post a Comment