Mwanaharakati wa kupigania haki
za wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya Binyavanga Wainaina amefariki dunia .
Nduguye James Wainaina amethibitisha kutokea kwa kifo hicho. Mwanaharakati huyo
amefariki akiwa na umri wa miaka 48. Nduguye Binyavanga amsema kuwa familia
yake inataka kusherehekea maisha yake , baada ya mwandishi huyo wa Kenya
kufariki usiku wa Jumanne alipokuwa akiugua. James alisema kuwa Binyavanga
hajakuwa katika afya nzuri katika kipindi cha miaka michache iliopita na hali
yake ilikuwa imedorora katika kipindi cha kati ya miezi miwili au mitatu.
Nduguye hatahivyo alikataa kufichua ugonjwa uliosababisha kifo chake. Wainaina
alikuwa mshindi wa tuzo ya Caine na aliorodheshwa na gazeti la Times magazine
miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani 2014. Amefariki siku mbili
tu kabla ya mahakama nchini Kenya kutoa uamuzi wa iwapo itafutilia mbali sheria
za kikoloni ambazo zinaharamisha haki za wapenzi wa jinsia moja.
SOURCE: BBC
0 Comments:
Post a Comment