Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), mkoa wa Kilimanjaro Ustaadh Awadhi Lema |
Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro Awadhi Lema, wakati alipokuwa akizungumza na Wanaandishi wa habaro ifisini kwake jana kuhusiana na mfungo wa Ramadhani.
Alisema wapo baadhi ya vikaba ambao wanatumia fursa hiyo kwa ajili ya kwenda kwenye majumba ya watu wakati wakiwa kwenye ibada usiku hivyo wanakuwa
“Tunalishauri jeshi la polisi liongeze nguvu katika kuimarisha ulinzi katika mfungo huu wa ramadhani kwenye misikiti yetu, jeshi la polisi tunalitegemea kwani tunaamini kila wakatri lipo imara tunaamini watatupa ulinzi wa kutosha,”alisema Lema.
Aidha Lema amewashauri Wafanyabiashara mkoani Kilimanjaro kuacha tabia ya kupandisha bei ya vyakula katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani , badala yake wauze bidhaa zao kwa bei rahisi ili kumsaidia wananchi kupata mahitaji kwa urahisi zaidi.
Lema alitumia fursa hiyo kuwashauri wafanyabiashara wasitumie mwezi wa ramadhani kwa ajili ya kupandisha bei ya vyakula kwa lengo la kuwakomoa Waislamu katika mfungo huo wa ramadhani.
“Naomba wafanyabiashara watumie mwezi huu ili kupata kipato kikubwa , wafanye bei ambayo ni rafiki ya vyakula ili Waislamu waweze kupata futari na mahitaji mengine yote,”alisema Lema.
Alisema endapo wafanyabishara watapandisha bidhaa hizo vinavyotumika kwa ajili ya futari katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani kutawapa ugumu Waislamu kutekeleza moja ya nguzo muhimu za ibada zao.
STORY &PHOTO BY: Kija Elias
0 Comments:
Post a Comment