Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Thursday, June 30, 2022

Zuberi Abdallah Kidumo: Meya mpya Manispaa ya Moshi

 

Meya wa Manispaa ya Moshi Zuberi Abdallah Kidumo, akizungumza na wajumbe wa baraza la madiwani muda mchache baada ya kukalia kiti hicho. 

Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro imepata Meya mpya wa kuiongoza manispaa hiyo baada ya songombingo la takribani miezi mitatu kufuatia kwa aliyeshika nafasi hiyo Juma Rahibu Juma kuvuliwa cheo hicho.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Rashid Gembe alimtangaza Zuberi Abdallah Kidumo kushika nafasi hiyo baada ya ushindi wa kura 27 kati ya 28 zilizopigwa na madiwani wa Manispaa hiyo.

Mwenyekiti wa mkutano huo maalum  Stuart Nkinda alianza kuongoza madiwani kupiga kura ya siri ya kumchagua Meya Zuberi Abdallah mnamo saa 4 za asubuhi ambapo kati yao madiwani wawili hawakuhudhuria kutokana na sababu mbalimbali.

Zuberi Abdallah ambaye ni diwani wa Njoro kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi alipambana na diwani wa Kiboroloni kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Frank Kagoma ambaye aliambulia kura moja.

Ushindi wa Zuberi Abdallah ni wa asilimia 96.4 wa kura zote zilizopigwa hasa ikizingatiwa kuwa katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2020 diwani pekee kutoka upinzani aliingia katika baraza hilo ambaye ni Frank Kagoma.

Mnamo Aprili 11, 2022 Manispaa ya Moshi ilimvua Umeya Juma Rahibu Juma kutokana na utovu wa nidhamu na kutumia cheo vibaya.

Akitoa shukrani zake baada ya kuapishwa rasmi kukalia kiti hicho Meya Zuberi Abdallah alisema, “Heshima hii kwangu naona kuwa ni deni, kwanza kabisa nimwombe Mwenyezi Mungu anijalie afya njema na awajalie nanyi afya njema ili tuweze kufikia yale malengo ambayo tumekuabaliana kuyafanya…tumeaminiwa na wananchi wetu.”

Zuberi Abdallah anakuwa meya wa nane kukalia kiti hicho tangu Moshi ilipopata hadhi ya kuwa Manispaa mnamo mwaka 1989.

Meya aliyevuliwa cheo hicho Juma Rahibu Juma akizungumza muda mchache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Meya mpya wa Manispaa ya Moshi mnamo Juni 30, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa manispaa hiyo.


Mameya walioingoza Manispaa ya Moshi

1989-1994 Abu Salim Mallya

1995-2000 Denis Chuwa

2001-2005 Lucas Tarimo

2006-2010 Lameck Kaaya

2011-2015 Jaffary Michael

2016-2020 Raymond Mboya

2020-2022 Juma Rahibu Juma

Diwani Aisha Agogo wa viti maalum katika Manispaa ya Moshi akipiga kura ya kumchagua Meya mpya mnamo Juni 30, 2022.