Bondia Ali Baba Ramadhani kutoka mkoa wa Kilimanjaro |
Masumbwi
au kwa majina mwengine ndondi au ngumi na kwa majina ya mitaani ndogwa, mawe
n.k. ni mchezo unapoendwa sana na watu wengi. Aidha mchezo huu ni kati ya
michezo inayoogopwa sana duniani.
Mchezo
wa ngumi uko hatarini kupoteza maana yake ya asili yaani kucheza kama burudani,
kuwakilisha nchi na kujenga ushupavu wa mchezaji.
Mamilioni
ya watu wanaojazana kuutazama wasingependa kabisa kujiingiza kuucheza mchezo wa
ngumi
Katika
kuucheza mchezo wa ngumi wachezaji wawili wanapanda kwenye ulingo
uliozungushiwa kamba tatu au nne. Mara nyingi vipimo vya ulingo vinatofautiana
kati ya ngumi za ridhaa na kulipwa. Lakini pamoja na tofauti hizo vipimo vya
ulingo huanzia futi 12 hadi 20 nikiwa na maana ya 12 kwa 12 za mraba na
kuendelea mpaka 20 kwa 20.
Ulingo
mwingi wa ngumi za ridhaa ni futi 17 kwa 17 ambapo wa ngumi za kulipwa huwa ni
18 kwa 18. Lakini ulingo unaotumika kwa mapambano ya ngumi za uzito wa juu huwa
kati ya futi 18 kwa 18 au 20 kwa 20!
Mchezo
wa ngumi huwakutanisha mabondia wawili waliovaa glovu mikono yote miwili zenye
uzito sawa kufuatana na uzito wao. Mabondia hawa hurushiana masumbwi kwenye sehemu
zilizokubalika. Sehemu hizi zinaanzia juu ya mkanda kiunoni hadi utosini.
Bondia haruhusiwi kumpiga mwingine kwenye kisogo.
Mabondia
wote wanatakiwa warushe ngumi zilizokunjwa vizuri na zinazopiga eneo
lililolengwa barabara. Kuna majaji watatu ambao wanatakiwa wakae kwenye pembe
tatu chini ya ulingo.
Hawa
ndio watakuwa wanatoa pointi kwa kila bondia kufuatana na uchezaji wake. Kwenye
ngumi za ridhaa pointi huwa zinatolewa kwa
kompyuta baada ya jaji mhusika kubonyeza kidude fulani kila bondia anapompiga
mwenzie.
Katika
ngumi za kulipwa majaji wanatakiwa waangalie jinsi mabondia wanapocheza na
kutoa pointi kufuatana na wanavyocheza. Baada ya kila raundi bondia aliyeshinda
hupewa pointi 10 dhidi ya 9 za aliyeshindwa.
Kama
bondia mmoja aliangushwa au kuhesabiwa wakati akicheza kwa sababu ya kupigwa
sana, pointi zake zinaweza kuwa 10 kwa aliyeshinda na 8 au 7 kwa aliyeshindwa
raundi.
Kila
baada ya raundi raferii hupita kwa kila jaji na kuchukua vifaratasi wanavyotumia
kutoa pointi na kumpelekea kamisaa wa pambano ambaye kwa kawaida hujumlisha
pointi za kila raundi na kutangaza mshindi. Refarii ndiye anayeweza kuamuru
bondia akatwe pointi anapoona kuwa amecheza rafu!
Mbali
na refarii na majaji kuna Kamisaa anayesimamia pambano na kujumlisha pointi
zote toka kila jaji ili kumpata mshindi. Kamisaa ndiye kwa kawaida hutoa
mshindi atakayetangazwa.
Mpiga
kengele ambaye hutakiwa apige kengele kila raundi inapoanza na inapomalizika.
Mtunza muda (Timekeeper) anayeangalia muda unaotumika kucheza na kupumzika kila
raundi ya pambano.
Watu
wengine muhimu kwenye mpambano ni makocha na masekonda wa kila bondia. Watu
hawa husimama kwenye kona ya kila bondia kumpa huduma muhimu kama maji,
kumfukuzia hewa, kumfuta jasho na kumpa ushauri wa alivyocheza raundi iliyoisha na mawaidha ya
jinsi atakavyocheza kila baada ya raundi.
Kuna
pia madaktari ambao hutoa huduma kwa bondia wakati wa mpambano. Daktari pia ana
uwezo wa kumshauri refarii amalize mpambano anapoona kwamba mmoja wa mabondia
anaumia vibaya na maisha yake yapo hatarini.
Cutman ni mtu anayemhudumia
bondia kwenye sehemu zilizokatika kichwani. Mara nyingi cutman ni watu walio na
uwezo wa kuziponyeza mikatiko isitoe damu na kumdhuru bondia asiweze kuendelea
na mpambano.
Katika nchi zilizoendelea
kama nchi za Ulaya, Amerika, Asia na hata Afrika ya kusini karibu kila bondia
ana Cutman wake. Hii inatokana na umuhimu wa kumjua bondia vizuri na umbile la
uso wake hivyo kuifanya kazi ya cutman kuwa raisi kidogo. Cutman anajua fika
jinsi ya kuziziba (kuzuia damu isitoke) majeraha ya usoni ya bondia wake.
Imetayarishwa na Jabir
Johnson kwa msaada wa Onesmo Ngowi, mtalaamu wa Masuala ya Ngumi nchini
Tanzania, Desemba 22, 2019. Baruapepe: jaizmelanews@gmail.com
Hamasa ya kupenda mchezo wa ngumi inatakiwa ianzie utotoni |
0 Comments:
Post a Comment