Wednesday, December 11, 2019

Ghana ni taifa la namna gani?



Ghana ni jina ambalo lina maana ya ‘Mfalme Askari’ likiwa limechukuliwa kutoka katika wafalme wa kipindi cha dola ya Ghana miaka ya 700 hadi 1240.

Ghana limetokana na wenyeji wanaozungumza Kisoninke. Lugha ya Kisoninke ni miongoni mwa lugha maarufu sana Afrika Maghariki ikiwa na takribani wazungumzaji milioni mbili kutoka Senegal, Ivory Coast, The Gambia, Mauritania, Guinea-Bissau, Guinea na Ghana.

Wakati huo dola ya Ghana ilikuwa ikikamata baadhi ya eneo kubwa kwa sasa ni nchi za Mauritania na Mali.

Hivyo basi kuwapo kwa nchi ya Ghana kumetokana na mzizi huo wa historia. Ghana ni taifa ambalo linapatikana Afrika Magharibi katika Ghuba ya Guinea likiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 238,535.

Taifa hilo limepakana na Ivory Coast kwa upande wa Magharibi; Burkina Faso kwa upande wa kaskazini, Togo kwa upande wa Mashariki na Ghuba ya Guinea na Bahari ya Atlantiki kwa upande wa Kusini.

Eneo ambalo ipo Ghana kwa sasa linaanzia katika karne ya 11 wakati wa kuimarika kwa Ufalme wa Ashanti.

Kuanzia karne ya 15 watu kutoka barani Ulaya walianza kuingia humo na kuanza masuala ya biashara. Katika karne ya 19 Waingereza walishika hatamu za eneo hilo na kuipa jina la British Gold Coast.

Mipaka ya sasa iliwekwa mwanzoni mwa miaka ya 1900. Ghana ilipata uhuru wake Machi 3, 1957.

Ghana  ina takribani watu milioni 30  wanaouzungumza lugha zao. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2010 ilionyesha asilimia 71.2 ni wakristo, asilimia 17.6 na asilimia 5.2 wanaabudu dini za asili. Ina milima, misitu na savanna.

Mji Mkuu wa Ghana ni Accra.

Imetayarishwa na Jabir Johnson..............................Desemba 11, 2019

0 Comments:

Post a Comment