ACP Said Hamduni |
Zaidi
ya abiria 100 wamenusurika kifo baada ya basi la Kampuni ya Harambee iliyokuwa
inatokea Arusha kufeli breki na kuyaparamia magari sita ya abiria katikati ya
mzunguko wa benki ya CRDB mjini Moshi na kusababisha majeruhi.
Kamishna
Msaidizi wa Polisi mkoa Kilimanjaro Salumu Hamduni alisema kuwa basi la Kampuni
ya harembee ilifeli breki na kuyaparamia magari zaidi sita na kusababisha ajali
na majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa
katika Hospitali ya KCMC na Hospital ya Mawenzi.
Hamduni
alisema ajali imetokea majira ya saa kumi na mbili jioni na kwamba jeshi la
Polisi inaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kwamba hakuna vifo.
Baadhi
ya manusura wa ajali hiyo walisema kuwa basi hilo ilikuwa na mwendo wa kawaida
ambapo dereva wa basi la Harambee baada ya kushindwa kulimudu alianza kupiga
kelele.
0 Comments:
Post a Comment