Desemba 11, 1943 alizaliwa mwanasiasa wa nchini Marekani John
Kerry. Jina lake halisi ni John Forbes Kerry ambaye alihudumu kama seneta kwa
tiketi ya chama cha Democratic kutoka mwaka 1985 hadi 2013.
Kerry aliingia
katika kinyang’anyiro cha kuteuliwa kugombea urais wa Marekani mnamo mwaka 2004
na baadaye mwaka 2013 hadi 2017 alikuwa Katibu Mkuu kiongozi wa Ikulu ya
Marekani wakati wa Utawala wa Rais Barack Obama.
Kerry alizaliwa katika
hospitali ya kijeshi ya Denver nchini Marekani kwa baba yake Richard Kerry
aliyekuwa rubani na mwanadiplomasia wa Marekani na mama yake Rosemary Forbes
Kerry ambaye alikuwa mtoto wa familia ya kitajiri ya Forbes iliyokuwapo huko
Boston kutoka katika uzao wa John Winthrop aliyekuwa gavana wa kwanza wa
Massachussets Bay.
Kerry alisoma huko New England na Uswisi na akapata
mafanikio makubwa akiwa shuleni na mwanamichezo kabla hajaingia katika siasa.
Baada ya kumaliza chuo kikuu cha Yale mwaka 1966 alikuwamo katika orodha ya
wanajeshi wa majini na hivyo aliungana na wanajeshi wengine katika vita vya Vietnam
akiwa ofisi wa boti ya kivita katika Delta ya Mekong.
Alirudi nchini Marekani
mwaka 1969 akitokea Vietnam na kutunukiwa cheo cha Luteni na Nyota ya Fedha,
Nyota ya Shaba na Nembo tatu za Purple Hearts. Mwaka 1970 alisimama kulitumikia
jeshi.
Alimuoa Julia Throne mnamo mwaka 1970 na uhusiano wake na mwanamke huyo
ulikoma mnamo mwaka 1988.
Mnamo mwaka 1995 alimuoa Teresa Heinz, alikuwa mjane wa
John Heinz seneta wa Pennsylvania na mrithi wa Heinz Company.
Mnamo mwaka 1976
alihitimu katika Shule ya Sheria ya Boston na kuwa mwanasheria msaidizi wa Kaunti
ya Middlesex huko Massachussets.
Akiwa
huko alipata umaarufu mkubwa katika kesi mbalimbali za jinai. Mnamo mwaka 1982
alirudi katika siasa na kuchaguliwa kuwa Luteni gavana wa Massachussets na
mnamo mwaka 1984 alishinda uchaguzi wa baraza la Seneti.
Kerry amechaguliwa
mara tatu 1990, 1996 na 2002.
0 Comments:
Post a Comment