Timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars imeshida
mchezo wake wa kwanza mbele ya Zanzibar Heroes kwenye michuano ya Afrika
Mashariki na Kati (Cecafa) Desemba 10, 2019 jijini Kampala.
Mchezo wa kwanza wa ufunguzi Kilimanjaro Stars ilipoteza kwa
kuchapwa bao 1-0 na Kenya lililopachikwa dakika ya nne.
Bao pekee la Kilimanjaro limepachikwa dakika ya 39 baada ya
mlinda mlango wa Zanzibar Heroes kuutema mpira uliopigwa na Eliuter Mpepo ukakutana
na Ditram Nchimbi ndani ya 18.
Michuano hiyo inafanyika nchini Uganda ambapo kwenye mchezo
mwingine Kenya ilishinda bao 2-1 dhidi ya Sudan.
0 Comments:
Post a Comment