Zaidi ya watu 14 wameuawa kwa
risasi ndani ya kanisa moja jana jumapili nchini Burkina Faso na askari wa Kiislamu
wenye msimamo mkali.
Wahanga wa tukio hilo
waliuawa na askari hao wakiwa katika ibada yao ya Jumapili mjini Hantoukoura
uliopo Mashariki mwa Brukina Faso.
Imedaiwa kuwa chanzo cha
waumini hao kuuawa haijawekwa wazi huku wauaji hao wakitoroka kwa pikipiki
baada ya kutenda unyama huo.
Mamia ya watu wamekuwa
wakiuawa nchini humo kwa miaka ya hivi karibuni wengi wao wakiuawa na makundi
ya Jihad, mapigano ya kikabila karibu na mpaka wa taifa hilo na Mali.
Serikali ya mkoanchini humo
imesema watu wengi wamejeruhiwa katika tukio hilo. Vyombo vya usalama nchini
humo vimesema miongoni mwa waliouawa ni mchungaji na watoto wake.
Mwezi Oktoba mwaka huu watu
15 waliuawa na wengine wawili walijeruhiwa katika shambulio lililofanywa katika
msikiti mmoja.
Mashambulio yanayofanywa na
waislamu wenye msimamo mkali yamekuwa yakiongeza
tangu mwaka 2015 huku maelfu ya shule zikilazimishwa kufungwa.
CHANZO: BBC
0 Comments:
Post a Comment