Shirika lisilo la kiserikali
linalojihusisha na watu walioumia uti wa mgongo SONGA MBELE, limetoa wito kwa
serikali na wadau wake, kulitambua kundi hilo la walemavu kwenye mapambano ya
virusi vya ukimwi.
Wito huo umetolewa Desemba 9, 2019 na
Mkurugenzi wa shirika hilo Faustina Urassa alisema watu wenye ulemavu wa uti wa
mgongo serikali imewaweka kando katika mapambo dhidi ya mapambano ya ugonjwa
huo.
“Tupende kuiambia jamii na serikali
pia, sisi kama watu wenye ulemavu wa uti wa mgongo tuko tayari kuwa moja
wapo katika jitihada za kupunguza mambukizi ya VVU , lakini jamii imekuwa
ikituona sisi wenye ulemavu hatuwezi kupata ukimwi jambo ambalo si
kweli,”alisema Urassa.
Katika hatua nyingine Urassa
aliitaka serikali na wadau wengine kuwezesha upatikanaji wa takwimu sahihi kwa
watu wenye ulemavu zinazoonyesha kiwango cha maambukiziya Ukimwi
kwa watu wenye ulemavu ili kupata muelekeo wa mapambano ya
maambukizi kwa kundi hilo.
“Napenda kutoa wito kwa
mashirika mengine pia na serikali kwa ujumla tunahitaji kuwepo na takwimu
zinazoonyesha kwamba watu wenye ulemavu wanapata maambukizi ya ukimwi kwa kiasi
gani,”alisema.
Alifafanua kwamba vijana wengi
wameathirika sana hivyo wanapofanya tafiti zao ni vyema wakaonyesha ni kwa
kiasi gani kundi la watu wenye ulemavu wameathirika kwa kiwango gani ili waweze
kujitambua na kuweza kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.
Kwa upande wao washiriki wa semina
hiyo iliyoandaliwa na shiurika hilo la SONGA MBELE la UMATI, Adamu Massawe na
Joyce Kimario wamesisitiza umuhimu wa elimu ya ukimwi kwa jamii inayoishi
maeneo ya vijijini.
“Tuoimbe Serikali iweze kuongeeza
juhudi za kutoa elimu ya ukimwi kwa watu wenye ulemavu, hususan katika maeneo
ya vijijini kwa sababu wengi elimu hii haijawafikia
vizuri hasa wenye ulemavu ambao wako maeneo ya vijijini.
STORY BY: Kija Elias
DATE: 11-12-2019
0 Comments:
Post a Comment