Mamadou Koulibaly kiongozi wa chama cha Upinzani cha Lider nchini Ivory Coast. |
Mwanasiasa wa chama cha upinzani nchini Ivory Coast amesema serikali imemfukuza nchini humo mmojawapo wa washauri wake muhimu katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa Urais nchini humo hapo mwakani.
Kiongozi wa Chama cha Upinzani cha Lider nchini humo Mamadou Koulibaly amesema mshauri wake mzaliwa wa Uswisi-Kameruni Nathaniel Yamb alitua jijini Zurich, Uswisi Jumatatu usiku baada ya kutakiwa kuondoka na mamlaka za nchi hiyo.
Koulibaly amesema serikali imekuwa na uwoga juu ya mshauri huyo. Kwa upande wake Yamb ameandika katika akaunti yake ya Twitter kuwa wananchi wa Ivory Coast wanaendeshwa kikabila hali ambayo imekuwa ikiwanyima haki zao.
Mapema mwaka huu waziri mkuu wa zamani wa taifa hilo alitupwa jela mwaka mmoja kwa kitendo cha kueneza habari za uongo kwa kutumia akaunti yake ya Twitter kuhusu serikali ya Rais Alassane Ouattara ambayo imekuwa ikiogopa kukosolewa hadharani.
Koulibaly ambaye ni spika wa zamani wa bunge la enzi za Rais wa zamani Laurent Gbagbo amekuwa mtu wa kwanza kutangaza kuwania Urais katika uchaguzi mkuu ujao katika taifa hilo kongwe na mahiri kwa zao la Kakao.
CHANZO: BLOOMBERG
0 Comments:
Post a Comment