Muziki wa Afro-Cuban Jazz
ni miongoni mwa mazao ya muziki wa Cuba na pia ni miongoni mwa muziki wa
mwanzoni kabisa katika Latin Jazz.
Tunapozungumza kuhusu Muziki wa Cuba
tunaingiza vyombo vya muziki wenyewe na muundo wa uchezaji wake ukitumia vifaa
vya kipekee vya asili ya watu wa Cuba.
Ikumbukwe kwamba muziki wa Cuba umekua
kutokana na ujio wa watu kutoka Afrika Magharibi na barani Ulaya hususani
Hispania.
Afro-Cuban Jazz ilianza mwanzoni mwa miaka 1940 wakati ambao Charanga
ilikuwa maarufu katika ardhi ya Cuba.
Wanamuziki wa Cuba Mario Bauza (Aprili
28, 1911-Julai 11,1993) na Frank Grillo ‘Machito’ (Februar 16, 1908 – Aprili
19, 1984) ndio waanzilishi wakuu wa Afro-Cuban Jazz. Wasanii hawa waliupeleka
muziki huo jijini New York ukiwa na vionjo vya mila na desturi za watu wa Cuba.
Mnamo mwaka 1947 walikutana na wasanii
wengine ambao walikuwa mahiri katika kutumia vyombo akiwa mpiga tarumbeta Dizz
Gillespie na mpiga percussion Chano Pozo.
Dizz na Chano waliongeza vyombo
vingine Tumbadora na Bongo katika Afro-Cuban Jazz iliyokuwa imejikita katika
Pwani ya Mashariki ya Marekani.
Bauza aliuwa mpiga wa Saxofoni, clarinet,
tarumbeta pia mtunzi na mwimbaji wa muziki wa Afro-Cuban Jazz. Katika miongo ya
mwanzoni Afro-Cuban Jazz ilikuwa na nguvu sana nchini Marekani kuliko hata Cuba
kwenyewe.
Mwanzoni mwa miaka ya 1970 Kenny Dorham akiwa na Orquesta Cubana de
Musica Moderna na baadaye Irakere walirudisha muziki huo katika ardhi ya Cuba.
Joe Henderson alikusanya kazi za Kenny Dorham na kuziweka pamoja mnamo mwaka
1963 ambapo mkusanyiko huo wa pamoja aliuita Blue Bossa kwenye albamu ya Page
One. Dorham aliurudisha Cuba ukiwa na staili (muundo) uliowavutia wengi wa
Songo.
Dorham alizaliwa Agosti 30, 1924 Fairfield katika kaunti ya Freestone
jimboni Texas nchini Marekani na kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 48,
mnamo Desemba 5, 1972 jijini New York.
Dorham alifanikiwa licha ya kutopewa
nafasi ya kutambulika sana lakini alionyesha uwezo wake wa Afro-Cuban Jazz ya
kutumia vifaa pekee yake (instrumental).
Imetayarishwa na Jabir
Johnson.......Desemba 28, 2019.
Mario Bauza (1911-1993) |
Frank Grillo 'Machito' (1908-1984) |
Kenny Dorham (1924-1972) |
0 Comments:
Post a Comment