Kuelekea ufunguzi
wa African Football League (AFL) ambao utafanyika Oktoba 20 mwaka huu jijini
Dar es Salaam, Mashabiki wa Simba wilayani Moshi Vijijini wameamua kwa moyo wa
dhati kujiandikisha kwa ajili ya kufungua tawi ambalo litawawezesha kuanza
safari ya kuwa wanachama rasmi wa klabu hiyo.
Akizungumza
na mashabiki wa klabu ya Simba wa Weruweru-Chekereni wilayani Moshi Vijijini
Katibu wa Simba SC mkoa wa Kilimanjaro Lawrence Monyonyi amesema ili kuwa na
uanachama katika klabu hiyo ni lazima kuanzia hatua ya matawi.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa muda wa mchakato wa kuanzisha tawi hilo Ali Mgaza amesema
wameamua kufanya hivyo kwa manufaa ya wapenda soka na Simba kwa ujumla
EATV
imezungumza na mashabiki wa Simba katika mkutano huo ambao ulianza na semina
namna ya kuwa mwanachama halali kwa mujibu wa Katiba ya Simba Toleo la 2018
Ibara ya
Pili (b)ya Katiba ya Simba SC ya mwaka
2018 kifungu kidogo cha kwanza kinasema malengo ya klabu ni kuwa chombo ambacho
wadau wenye tamaduni na itikadi sawa za kimichezo, watakusanyika pamoja,
kutengeneza umoja kupitia mfumo wa uanachama, na kupitia umoja huo waweze
kuunganisha nyenzo zao na kuwa wamiliki wa hisa katika kampuni ya Simba Sports
Club Company Limited.
0 Comments:
Post a Comment