BOMANG’OMBE,
KILIMANJARO
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman
Kinana amewataka wanachama wa chama hicho kuacha tabia ya kuwania nafasi za
uongozi pindi wanapoona aliyepo madarakani anaendelea kufanya vizuri.
Akizungumza na wanachama hao katika Mkutano Maalum wa Jimbo
la Hai uliondaliwa na mbunge wa jimbo hilo Saashisha Mafue wa kuwasilisha
utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka mitatu kutoka 2020 hadi 2022
uliofanyika kwenye Ukumbi wa Dream Park mjini Bomang’ombe, Hai; Kinana amesema
kiongozi anayefanya vizuri akiwa madarakani ni faraja na ukombozi kwa wananchi
wake.
Awali Kinana aliwasili katika Ofisi za CCM Hai kwa ajili ya
kuzungumza na viongozi wa chama hicho mkoa wa Kilimanjaro kabla ya kwenda
katika ukumbi wa Dream Park na kuzungumza na hadhira ya wanachama.
Viongozi wa dini na kimila walialikwa katika Mkutano huo
Maalum wa Utoaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya
Jimbo la Hai kutoka Novemba 2020 hadi Oktoba 2022.
Kwa upande wake Mbunge Mafuwe amesema kuanzia Novemba 2020
hadi Oktoba 2022 Halmashauri ya Hai ilishapokea jumla shilingi bilioni tatu
(3,715,520,202.94) kutoka serikali kuu kwa ajili ya shughuli mbalimbali za
maendeleo katika jimbo hilo.
USULI WA JIMBO LA HAI, KILIMANJARO
Jimbo la Hai lipo kanda ya Kaskazini Mashariki mwa nchi ya
Tanzania mkoani Kilimanjaro likiwa na ukubwa wa Kilometa za Maraba 1011 sawa na
hekta 101,000. Kati ya hizo hekta 73,803 ni eneo la makazi, shughuliza kilimo
na ufugaji na hekta 27, 297 ni eneo la msitu na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
0 Comments:
Post a Comment