Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwanaume mmoja mkazi wa Wilaya ya Same, kwa tuhuma ya kupatikana na vipande sita ya meno ya tembo.
Katika taarifa iliyotolewa Machi 14,2023 na Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani hapa ACP Simon Maigwa, mbele ya waandishi wa habari imeeleza kuwa jeshi hilo walifanikiwa kukamata meno hayo ya tembo sita kutoka kwa wasamaria wema ambao walitoa taarifa hiyo kwa jesho la polisi.
ACP Maigwa amesema mtuhumiwa huyo ambaye alikamatwa wilayani Same , atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapaokamilika ambapo watashirikiana na Ofisi ya Wanyamapori kujua thamani ya meno hayo.
Katika tukio lingine jeshi hilo limekamata gari moja aina ya Toyota Land Cruiser Prado TX inayodhaniwa kuwa ya wizi iliyokuwa imebandikwa namba za usajili T 929 DFH na baada ya kuikagua gari hiyo kwa kina ilibaimika kuwa na namba za usajili wa nchini Kenya KDH 554 A kwenye vioo vyake.
Aidha jeshi hilo limekamata kompyuta mpakato (Laptop) 27, Televishen Nne, Flat Screen, Monitor ya kompyuta moja na simu tano aina ya iPhone moja na Samsung 4 zilizoibiwa kwenye matukio tofauti.
Katika operesheni za madawa ya kulevya na pombe haramau ya gongo jeshi hilo limesema jumla ya watuhumiwa 161 wa kesi za madawa ya kulevya na pombe haramu ya gongo walikamatwa
Amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Februari mwaka huu wamefanikiwa kukamata pikipiki 15 zinazodhaniwa kuwa za wizi.
0 Comments:
Post a Comment