Thursday, March 23, 2023

RC BABU: Wataalamu wa Afya simamieni kikamilifu ukusanyaji mapato vituo vya afya

Wataalamu wa Afya mkoa wa Kilimanjaro katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Wakurugenzi watendaji wa halmashauri,  Wafamasia, Waratibu wa maabarq, maafisa.manunuzi na Wataalam waTehama, yanayotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) yanayohusu mfumo wa Kieletroniki wa ugavi wa bidhaa za afya. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliwakilishwa na Katibu Tawala Dk Vedasto Makota mnamo Machi 23, 2023. (Picha na Kija Elias/KILIMANJARO)

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu,  amewataka Wataalam wa Afya toka Halmashauri zote za  mkoa huo, kusimamia kikamikifu ukusanyaji wa mapato katika vituo vya kutolea huduma ya Afya ili waweze kuwalipa Washitiri kwa wakati baada ya kupokea shehena ya bidhaa za afya na kuepuka madeni yasiyoyalazima.

Pia mkuu huyo wa  mkoa ametoa maelekezo  kwa Wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa huo, kusimamia kikamilifu afua mbalimbali za mfumo wa ugavi wa bidhaa afya ili kupunguza changamoto zinazotokana na usimamizi mbovu wa bidhaa hizo.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Dk Vedasto Makota ametoa wito huo Machi 23,2023 wakati  wa ufunguzi wa mafunzo;

Kwa Wakurugenzi watendaji wa halmashauri,  Wafamasia, Waratibu wa maabarq, maafisa.manunuzi na Wataalam waTehama, yanayotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) yanayohusu mfumo wa Kieletroniki wa ugavi wa bidhaa za afya.

Dk. Makota amesema kuwepo kwa Washitiri ni utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020 ambayo inataka hospitali zote Nchini zihakikishe zinakuwa na dawa hivyo kwenye Bohari za Dawa (MSD) zinapopungukiwa au kutokuwa na dawa na vifaa tiba lazima kuwepo na wasambazaji wengine watakaotoa huduma hiyo.

Makota amesema mfumo huo  utarahisisha upatikanaji wa bidhaa za Afya zitakazokosekana katika bohari za madawa (MSD) ili kuimarisha na kurahisisha upatikanaji wa bidhaa hizo katika vituo vya kutolea huduma za afya Nchini jambo ambalo limekuwa ni changamoto.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Uratibu wa Kitaifa ya Mfumo wa Mshitiri  kutoka TAMISEMI Amiri Mhando, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwezesha upatikanaji wa huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Mhando amesema mfumo huo wa Kieletroniki una uwezo wa kuona taarifa kwa haraka za ufanyaji kazi wa Mshitiri na kubaini uwezo wake kwa kutimiza mahitaji ambayo vituo vya afya au zahanati walikuwa wakipata,"amesema Mhando.

Naye Mtaalamu wa huduma za maabara mkoa wa Kilimanjaro Rachel Mkandya, amesema mfumo wa mwanzo waliokuwa wakiutumia ulikuwa ukichukua muda wa siku 14 hadi mwezi, kuwepo.kwa mfumo huo wa Kieletroniki utakwenda kurahisisha upatikanaji wa dawa, uagizaji wa vifaa tiba na vitenganishi kwenye vituo.

Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Dk. Mtikija Msuya, amesema mfumo huo utakuwa na tija kwa wananchi kutokana na kuwepo kwa upatikanaji wa dawa kwa urahisi ikiwa bohari za dawa hazitakuwa na bidhaa za afya, huduma hiyo itakuwa na Washitiri ambao watakuwa wasambazaji.
Mhudumu wa Afya katika mojawapo ya Kituo cha Afya nchini Tanzania. (PICHA kwa hisani ya gazeti la DAILY NEWS)


0 Comments:

Post a Comment