Akizungumza
na Jaizmela News Onesmo Alfred Ngowi alisema tasnia ya ndondi imekuwa
ikikabiliwa na changamoto lukuki kutokana na ukosefu wa sheria za kuendesha
ngumi za kulipwa.
“Kuna
tatizo kubwa sana ambalo linapaswa kutatuliwa kwa haraka zaidi, kwa mfano
nchini Tanzania Mfumo wake wa ngumi
hususani wa michezo yote ya kulipwa ni lazima iweze kutungiwa sheria, kwani kwa
sasa hivi hakuna sheria ya kuendesha ngumi za kulipwa au michezo ya kulipwa
hapa nchini, bali kuna Sera ambayo ilitungwa bila kushirikisha wà dau wote wa
michezo ya kulipwa,” amesema Ngowi.
Rais wa World Alliance Boxing Association (WABA) Onesmo Ngowi |
Ngowi
alisema kinachofanyika kwa sasa nchini ni sera tu inayotumika katika kuendesha
ngumi za kulipwa.
“Tunaiomba
Serikali kupitia Wizara inayohusika na michezo pamoja na taasisi zinazohusika
na michezo kupeleka hoja bungeni ya kutungwa kwa sheria itayosimamia michezo ya
kulipwa hapa nchini. Sheria hiyo itakapoundwa itakuwa na uwezo wa kusimamia
kwa.usahihi tasnia ya ngumi za kulipwa kuanzia Uaandaji, kumlinda bondia
mwenyewe, ili aweze kupata haki zake,” ameongeza Ngowi.
Ngowi
alisema mapromota walio wengi wamekuwa wakiandaa mapambano ya ndondi na
kuwalipa ujira kidogo mabaondia kutokana
na uksoefu wa sheria na mikataba thabiti.
“Lazima
kuwe na sheria inayosema mkuzaji (Promoter) anatakiwa.kuwa na sifa zipi ,
afanyeje ili aweze kuanza kupromoti ngumi, hapa nchini, analindwaje katika
sheria hiyo, bondia anapoumia akiwa mchezoni anatakiwa kupata msaada gani,
akishastaafu ngumi atakuwa akipata msaada gani,
bondia analindwaje katika mikataba hiyo , viwango vya kutoa fedha
kwa bondia, kucheza katika mapambano zinatakiwa
kuanzia viwango gani,” amesema.
Aidha
Ngowi aliweka bayana suala la mabondia weusi wanaopambana katika nje ya bara la
Afrika kuwa wamekuwa wakinyimwa fursa
nyingi za kushiriki mashindano ya ngumi huku akisisitiza kuwa bado ubaguzi wa
rangi michezoni hususani katika ngumi haujatokomea kwa kiwango cha kuridhisha.
Hata
hivyo Ngowi alisema uwepo wa WABA umesaidia pakubwa kwa mabondia wa Kiafrika kupata
fursa za kushiriki mashindano ya ngumi ikilinganishwa na hapo kabla ya
uanzishwaji wa Shirikisho hilo la Vyama vya Ngumi Duniani.
“Mabondia
wengi duniani hususan weusi wamekuwa wakitumika kama chombo cha kutengeneza
ulaji kwa mabondia wa kizungu, weusi wamekuwa wakiishi maisha ya dhiki sana,
mpaka sasa nchi 99 zimmeshiriki katika mapambano ya ngumi tangu kuanzishwa kwa
WABA mnamo mwaka 2005.
Ngowi
alisisitiza kuwa WABA imekuja na mkakati wa kuwatengenezea bima za maisha,
kuumwa, mafao yaoa pindi wanapostaafu waweze kulipwa, lakini pia mabondia
watakao kuwa wakishiriki kwenye kwenye mapambano makubwa waweze kupata stahiki
zao ili kuweza kuendesha maisha yao na ya familia zao.
0 Comments:
Post a Comment