Mkuu wa Chuo hicho Profesa Jaffari Kideghesho, aliyasema hayo jana wakati akizungumzana waandishi wa habari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanyapori duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 3 ambapo siku hiyo imewekwa mahususi ili kuhakikisha wanyamapori wanakaa katika mazingira mazuri na salama.
Alisema kama Wakufunzi wa Usimamizi wa Wanyamapori na Uhifadhi wa Mazingira, pia wameamua kuitumia siku hiyo ya wanyamapori duniani kutathmini changamoto zinazowakabili wanyamapori pamoja na viumbe vingine vilivyoko kwenye hifadhi zilizopo hapa nchini.
Prof. Kadeghesho amesema Wilaya ya Mwanga yako maeneo katika milima ya Tao la Mashariki hususan kwenye milima ya Upareni, eneo hilo bado halijafanyiwa kazi pamoja na mazingira yake kuwa rafiki kwa tafiti aina mbalimbali.
Amesema kama chuo chenye dhamana ya kutoa mafunzo ya usimamizi wa wanyamapori pamoja na uhifadhi wa mazingira watakwenda huko ili kubaini maeneo ambayo wanaweza kuyatumia kwa tafiti mbalimbali kwa ajili mafunzo na shughuli zingine za kitafiti zinazofanywa na chuo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Dk. Salehe Mkwizu amesema wilaya hiyo inalenga kuendeleza eneo hilo ili liwe kivutio cha utalii na hivyo kuongeza mapato ya halmashauri hiyo na wananchi wanaozunguma Tao hilo la Mashariki.
Mkwizu amesema pia shughuli hizo zitakuwa zinalenga kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kukuza utalii wa Taifa kupitia filamu ya Royal Tour Tanzania na ambazo zimeanza kuonyesha mafanikio makubwa hapa nchini.
Kwa upande wake Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo hicho Dk. Emmanuel Martin, amesema uongozi wa chuo cha Mweka kimetembelea wilaya ya Mwanga eneo la Kambi ya Nyani Kata ya Shighatini kwenye safu ya milima ya Taola Mashariki kwalengo la kujionea mazingira halisi ambapo jamii ya maeneo hayo imeshiriki kikamilifu kuyatunza
Martin ambaye pia ni Mhadhili Mwandamizi katika Idara ya Usimamizi wa Wanyamapori Mweka amesema eneo la Tao la Mashariki halijapata msukumo wa kutosha kwenye maswala ya tafiti mbalimbali kama ilivyo kwenye milima ya Usambara Mashariki na Magharibi, Uluguru pamoja na milima ya Udzungwa, hivyo kupitia tafiti ambazo chuo hicho kitakwenda kuzifanya kupitia Tao hilo la Mashariki zitasaidia kutanzautalii wa ndani.
Uweko wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA), na shughuli zake mbalimbali hapa nchini, mbali na faida za kitafiti kwa ajili ya mafunzo, pia uweko wao utasaidia kukuza uchumi wa eneo la Wilaya ya Mwanga kwani matokeo ya tafiti zao zitawezesha eneo la Kambi ya Nyani Kata ya Shighatini kwenye safu ya milima ya Taola Mashariki kuwa kivutio cha watalii kutembelea huko na hivyo kuongeza mapato ya wananchi, halmashauri na yale ya serikali kwa ujumla.
0 Comments:
Post a Comment