Wednesday, March 29, 2023

Wagonjwa wa Marburg marufuku kufanya tendo la ndoa

 

Baada ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuthibitisha visa vya wagonjwa wa Marburg mkoani Kagera ambako watu  watano kati ya wanane walifariki dunia kutokana na virusi  vya homa ya Marburg, sasa wa imebainika kuwa wagonjwa wa homa hiyo wanapaswa kujizuia kufanya tendoo la ndoa kwa mwaka mmoja.

Akizungumza na Jaizmela News Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto Dk. Leonard Subi, alisema, “Popo ambao wanapenda kuishi kwenye maeneo ya mapango na wanyama wengine kama swala, nyani na nguruwe wanaweza kuwaathiri binadamu kutokana na kuwa karibu na mnyama lakini pia kula nyama yake.”

Aidha Dk. Subi aliongeza, “ Unapoingia kwa binadamu virusi hivyo vinaweza kumwambukiza mtu mmoja hadi mwingvine kwa kugusana, kushikana mikono, majasho, mikono au kujami.”

Katika suala la kujamiana (kufanya tendo la ndoa) Dk. Subi alisema, “ sisi hatuzuii kujamiana kama watalaamu tunakushaurui njia nzuri ya kujamiana ili usimwambukize mwenza wako, kwanza kwa kufanya ufuatiliaji, mtu mwingine anaweza kuathirika kwa virusi vya Marburg bahati nzuri akapona sife, lakini bahati mbaya pia akaendelea kufanya tendo la ndoa baada ya siku 21 huwa tunamfanyia ufuatiliaji.

Dk. Subi alisisitiza kuwa virusi vya Marburg vinaweza kukaa katika shahawa kwa mwaka mzima hivyo hatari ya kuambukizwa ni kubwa wa waliothirika na wakapona.  

Hata hivyo Dk. Subi alisema Hospitali ya Kibong’oto imeshatuma wataalamu mkoani Kagera kwa ajili ya utafiti huku wengine wakiwa tayari endapo maradhi hayoi yatasambaa nchini.

Shirika la Afya Duniani WHO lilisema, “Mwonekano wa wagonjwa katika awamu hii umeelezewa kuwa unaonyesha sifa za kama mizimu, macho ya ndani,  nyuso zisizo na hisia na uchovu  mwingi.”

Mnamo Machi 21, 2023 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alisema serikali imefanikiwa kuuzuia ugonjwa huo kutoka nje ya mipaka ya ya mkoa wa Kagera.

Ugonjwa huo huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine au kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu na unatajwa kutokuwa na tiba bali hutibiwa kwa dalili husika anazokuwa nazo mtu.

Popo wa Matunda aina ya Rousette wa nchini Misri mara nyingi huwa na virusi. Nyani wa kijani kibichi na nguruwe wanaweza kubeba.

Miongoni mwa binadamu huenea kupitia maji ya mwili na malazi yaliyochaful;iwa nao na hata wakipona, damu au shahawa zao, kwa mfano zinaweza kuwaambukiza wengine kwa miezi mingine baadaye.

DALILI ZA MARBURG

Unaanza ghafla na Homa, Kuumwa vibaya kichwa, kuumwa misuli na baada ya siku tatu hufuatwa na kuharisha , kuumwa na tumbo, kichefuchefu na kutapika.



Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto Dk. Leonard Subi, akizungumza na waandishi wa Habari mnamo Machi 28, 2023 mjini Moshi.



0 Comments:

Post a Comment