Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) imetoa tani 256 za chakula kwa wananchi wa wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, hatua ambayo itasaidia kukabiliana na upungufu wa chakula wilayani humo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mwajuma Nasombe, ameyasema hayo.Machi 9,2023 wakati akitoa taarifa ya hali ya chakula wilayani humo kwenye Baraza la Madiwani wa wilaya hiyo.
Nasombe amesema chakula hicho kimenufaisha wananchi wa kata 16, ambapo kitawasaidia kupunguza makali ya mapungufu ya chakula ambayo yalitokana na kutokuweko kwa mvua za kutosha wakati wa vipindi vya masika na vuli mwaka jana kwani hata wale waliofanikiwa kulima, kile kidogo walichokuwa wanatarajia kukipata kiliharibiwa na tembo wavamizi.
Aidha Nasombe alikiambia kikao hicho kuwa, mbali na serikali kutow chakula hicho ziko baadhi ya taasisi za kidini pamoja na mashirika binafsi yaliungana na serikali katika kukabiliana na upungufu wa chakula wilayani humo kwa kutoa msaada wa vyakula mbalimbali.
Amesema taasisi ya World Vision iliungana na serikali kwa kutoa chakula kwa ajili ya chakula mchana kwa miezi mitatu, kwenye shule zote za msingi na sekondari zilizoko kwenye tarafa za Jipendee na Lembeni.
Amesema taasisi hiyo imeamua kutoa msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 179.5, baada ya kubaini ya kuwa wazazi wasingeweza kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao kutokana na kukosa mavuno na fedha za kuchangia chakula mashuleni.
Nasombe amesema kuwa kwa upande wa uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Mwanga (KKKT-Mwanga) umetoa msaada wa chakula cha mchana wenye tahamni ya shioingi milioni 300 kwa shule zilizoko kwenye kata tano zilizoko wilayani humo, ambazo amesema ni pamoja na kata ya Kwakoa, Toroha, Kigonigoni, Mgagao na Kivisini.
Amesema wananchi watakaonufaika na msaada hao ni wale wa Kwakoa katika kata ya Kwakoa, Simkizungu na Karambandea katika kata ya Toroha, Kwa kihindi, kata ya Kigonigoni, Pangalo na Kiverenge kata ya Mgagao na wale wa kijiji cha Kwanyange, kilichoko kata ya Kivisini na kongeza kuwa mchango huo unatarajia kuzinufaishaya kaya 700.
Akiongea katika kikao hicho Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mwanga Mshikizi Kanali Hamis Maigwa amezipongeza taasisi hizo kwa michango yao ya chakula ambapo amesema itasaidia kuwapa wanafunzi motisha wa kuendelea na masomo yao bila mashaka.
Aidha amewpaongeza madiwani wa halmashauri hiyo kwa mshikamano walio nao wakati wa kutekeleza majukumu yao jambao ambalo amesema limechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya kimaendeleo yanayopatikana wilayani humo ikiwemo haswa kwa upande wa makusanyo ya maduhuli ya serikali.
0 Comments:
Post a Comment