Wazazi na Walezi wametakiwa kuacha tabia ya kuwabagua watoto jambo ambalo limekuwa likileta chuki,matabaka na hupelekea kusababisha ukatili kati yao.
Hayo yamesemwa Machi 4 2023 na Afisa Ustawi wa Jamii Bi. Daines Simon anaye hudumu kwenye Makao ya Watoto na Vijana wenye mahitaji maalum cha (Kahe Home For Children And Youth's With Special Needs) kilichoko Kata ya Kahe Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati akizungumza na Redio Kicheko Live iliyotembelea kituo hicho ili kuweza kujua changamoto zinzokikabili chuo hicho.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kituo hicho Martha, Daines amesema kuwa wako baadhi ya Wazazi wamekuwa wakiwathamini watoto wenye uwezo na kuwaona watoto wasiokua nacho na wale wenye ulema hawana thamani na kusababisha uchonganishi.
Asilimia kubwa ya Ukatili wanaofanyiwa watoto huwa unaanza ngazi ya familia wakiwemo ndugu wa karibu wa baba au mama, huku wakati mwingine wamekuwa wakiwatishia watoto kutokusema juu ya vitendo wanavyowafanyia.
Akizungumzia changamoto ya kituo hicho Afisa Ustawi huyo amesema Kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo bweni kwa ajili ya kuwalaza watoto hao pamoja na kitanda kwa ajili ya watoa huduma ya kwanza.
Naye Mweka Hazina wa Kikundi cha Wanawake Wapambanaji Mjorohoni Prisila Alexander na Mjumbe wa kikundi hicho Coletha Shirima, waliotembelea kituo hicho kwa ajili ya kuangalia changamoto zinazo wakabili watoto hao.
Wameziomba familia zenye uwezo kuweza kuwasaidia watoto hao kwa kile walichonacho kwani kuwasaidia watoto hao ni thawabu kutoka kwa Mungu.
Kituo hicho kina jumla ya watoto 14 wenye mahitaji maalumu, wanasake 9 na wanaume 5 wanaotunzwa katika kituo hicho.
0 Comments:
Post a Comment