Wednesday, March 22, 2023

Mahafali ya Kidato cha Sita Wasabato-Hai 2023 yalivyofana, Dk. Subi mgeni rasmi

Vijana wa Kanisa la Waadventista (Wasabato), wametakiwa kuwa wazalendo na waaminifu kwa nchi yao ili kuwa kielelezo kwa jamii inayowazunguka.

Wito huo umetolewa na mchungaji Richard  Matoti wa kanisa la waadventisa Wasabato mtaa wa Hai, wakati wa Ibaada maalum ya kuwaombea wanafunzi wa kidato cha sita wanaotarajiwa kuanza kufanya mitihani yao mwaka huu.

Matoti amesema vijana ni tegemeo kubwa la kanisa  na taifa kwa ujumla hivyo wanapaswa kuwa na usafi wa maisha, usafi wa tabia ili wasiwe na maswali kanisani kwa jamii na  kwa wazazi wao.

Katika mahubiri yake mchungaji Matoti, amewaasa wanafunzi hao kuweka bidii katika kusoma sambamba na kusimama katika mwenendo ulio mwema kwa walimu na wazazi wao.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika mahafali ya Tano ya kidato cha sita shule ya  Sekondari Hai, Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto Dk. Leonard Subi, amesema vijana kama watalelewa kwenye misingi imara ya neno la Mungu, watakuwa wazalendo wazuri kwa nchi yao.

Aidha Dk. Subi  ameahidi kutoa kila mwisho wa mwezi kwa mwaka mzima kwenye sehemu ya mapato yake  kiasi cha 50,000 ili kuwawezesha viongozi wa dini ili waweze kupeleka uinjilishaji wa neno la  Mungu kwa vijana walioko mashuleni.

Awali wakisoma risala yao kwa mgeni rasimi wahitimu hao waneomba kuchangiwa fedha kwa ajili ya kupata Projector ambayo watakuwa wakiitumia katika kufundishia ujumbe wa neno la Mungu.

Jumuiya ya Wanafunzi wenye Imani ya Waadventista  ASA Tawi la shule ya Sekondari Hai ina jumla ya wanafunzi 78, ambapo katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza elimu yao ya kidato cha sita ni wahitimu 9.








0 Comments:

Post a Comment